Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, August 14, 2019

Mabalozi 42 wanaoiwakilisha Tanzania nje kutembelea mradi huu kwa pamoja!

Mabalozi 42 wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kutembelea mradi wa kihistoria wa kufua umeme wa maji ambao umepewa jina rasmi la Julius Nyerere Hydropower Unit, uliopo Rufiji mkoa wa Pwani.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Dkt. Hassan Abbas, amesema mabalozi hao ambao tayari wapo hapa nchini kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa jumuiya ya maendeleo SADC, watafanya ziara hiyo ili kuwawezesha kufanya diplomasia ya uchumi katika nchi walizopo kwa lengo la kuleta wawekezaji zaidi.
Aidha Dkt. Abbas amesema katika kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi za SADC, wa kwanza kuwasili nchini atakuwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye atawasili jumatano, kwanza kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini ambapo atapata fursa ya kutembelea eneo la kihistoria la Mazimbu Morogoro lenye historia ya pekee kwa ukombozi wa nchi za Afrika.

Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na serikali wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC umeanza hapa nchini ukitarajiwa kufikia kilele tarehe 17 na 18 ambapo viongozi wote wa nchi 16 wanachama wamethibitisha ushiriki.

No comments :

Post a Comment