Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 2, 2019

RC Ayoub awataka viongozi kuleta mabadiliko katika michezo!

Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka viongozi wa vyama vya michezo na wanamichezo mkoani humo kushirikiana na kuwa wamoja ili kuleta mabadiliko ya michezo.

Ayoub alieleza hayo katika mchezo wa ngao ya jamii ikiwa ni ufunguzi wa ligi  ya madaraja mbali mbali mkoani humo ukliozikutanisha timu za Baharia ya Marumbi na New Boys ya Paje uliochezwa katika uwanja wa Bungi wilaya ya Kati, Unguja.
Amesema kuanzishwa kwa mashindano ya ligi za mkoa kunakotokana na mabadiliko ya katiba ya shirikisho la soka Zanzibar (ZFF) kutasaidia kuleta mabadiliko katika mchezo wa mpira wa miguu katika mkoa huo hatua ambayo itazijengea uwezo wa kushiriki kwenye mashindano ya ngazi ya wilaya, mkoa na taifa.

“Nimeambiwa katika mkoa wetu hakuna timu hata moja inayoshiriki mashindano ya ngazi ya taifa. Timu zetu zote zinacheza madaraja ya chini, sasa ufunguzi wa mashindano haya natamani iwe chachu na chanzo kwa timu zetu kucheza katika mashindano ya ngazi ya taifa”, alisema Ayoub.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema serikali ya mkoa itahakikisha inatoa kila aina ya msaada kwenye michezo mbali mbali ukiwemo mchezo wa soka ili kuunga mkono sera ya taifa ya kuimarisha sekta ya michezo nchini.

“Wakati wote tutahakikisha tunashirikiana nanyi kukuza sekta ya michezo ndani ya mkoa ili kupiga hatua kubwa za maendeleo ya michezo lakini pia kuunga mkono jitihada za Rais wetu Dk. Ali Mohamed Shein ya kuleta vugu vugu la michezo nchini”, alisema Ayoub.

Aidha ayoub aliwahimiza wanamichezo kuendelea kufanya mazoezi ili kujiimarisha kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja kutokana na michezo kuwa chanzo cha ajira sambamba na kuimarisha umoja na mshikamano kati yao.

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa kusini unguja Shauri Hassan Ali alisema chama chake kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ofisi ya kuendeshea shughuli zao hatua ambayo inasababisha usumbufu kwa vilabu vinavyopatiwa huduma.

“Chama chetu kinakabiliwa na changamoto nyingi licha ya dhamana kubwa tuliyokabidhiwa ya kusimamia mpira wa miguu lakini kubwa ni ofisi ya kufanyia kazi zetu, hatujawa na mahali maalum”, alisema Shauri.

Nae nahodha wa timu ya Baharia ya Marumbi iliyoibuka washiondi wa mchezo huo, Mohammed Ali Choyani alisema ushindi huo umeongeza ari na hamasha kwa wachezaji wa timu yao hatua ambayo itaongeza uwezo wao katika msimu huu wa ligi.

 Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Kati Hamida Mussa Khamis alisema wilaya yake imeendelea kuimarika kwa kuwa na viwanja vya mpira wa miguu hatua ambayo inatanua wigo wa kuibua vipaji vya wachezaji wa mpira katika wilaya hiyo.

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na timu zinazoshiriki ligi za madaraja mbali mbali mkoani humo, Baharia ilifanikiwa kutwaa ngao hiyo baada ya kuibamiza New boys bao 1 – 0 lililofungwa na Steven Cosmas katika dakika ya 32 wakati ligi za mkoa huo zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Oktoba 5,  mwaka huu kwa kushirikisha timu 20.

No comments :

Post a Comment