dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 14, 2020

‘Hakuna tishio la Tsunami Tanzania’!

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema hakuna tishio la kutokea kwa mawimbi makubwa ya tsunami nchini humo kufuatia tetemeko la ardhi la Jumatano usiku.

Tetemeko la ukubwa wa kipimo cha 5.9 lilitokea saa mbili usiku baharini katika eneo lililopo kusini mashariki mwa Mkoa wa Pwani.
Kishindo cha tetemeko hilo kimeripotiwa katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam, Zanzibar na Mombasa, Kenya. Hata hivyo, hakuna madhara makubwa ya miundombinu ama kwa maisha ya binadamu yaliyoripotiwa kufuatia tukio hilo.

Kutokana na tetemeko hilo kutokea baharini, kumekuwa na hofu kuwa linaweza kusababisha mawimbi makubwa ya tsunami.

“...Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imefanya uchambuzi wa taarifa za tetemeko hilo katika kituo chake cha Tahadhari ya Tsunami ili kuona iwapo kuna uwezekano wowote wa tetemeko hilo kusababisha mawimbi ya Tsunami baharini. Matokeo ya uchambuzi huo yanaonesha kuwa hakuna tishio la Tsunami kutokana na tetemeko hilo,” imeeleza taarifa ya TMA.

Kwa mujibu wa TMA tetemeko hilo halikuwa nguvu kubwa na hakuna maporomoko ya ardhi yaliyojitokeza baharini ambayo yangeweza kuzalisha tsunami.

“Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawashauri watumiaji wa eneo la bahari ikiwa ni pamoja wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyokaribu na bahari ya Hindi kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli kwa kuzingatia taarifa ya hali ya hewa Baharini kama ilivyotolewa awali na Mamlaka.

BBC

No comments :

Post a Comment