dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 27, 2021

TLS yaingilia kati sakata la Freeman Mbowe!

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimeingilia kati sakata la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kikitaka aachiliwe au afikishwe kwenye mamlaka za kisheria.

Kiongozi huyo wa chama hicho, kikuu cha upinzani nchini, alitiwa mbaroni alfajiri ya kuamkia Julai 21 akiwa hoteli ya Kingdom mtaa wa Ghana alikokifikia kwa ajili ya kushiriki kongamano la Katiba Mpya lililoandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

Hata hivyo, siku iliyofuata Msemaji wa Polisi nchini, David Misime aliueleza umma kuwa Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.

Msimamo wa TLS umetolewa leo Jumapili Julai 25, 2021 na rais wa chama hicho, Dk Hoseah katika tamko lake lililosambazwa kwenye mitandao ya kijamii mbalimbali.

Akinukuu, Katiba ya Tanzania, Dk Hoseah amesema Ibara ya 21(1) inatoa haki ya kujumuika na Ibara ya 13(1) inatoa masharti ya watu wote kuwa sawa mbele ya sheria.

Dk Hoseah ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), amesema kitendo cha kumkamata usiku wa manane Mbowe na wenzake, kwa sababu ya kuandaa kongamano ni ukiukwaji wa Katiba na sheria za nchi.

Amesema kufanya kongamano haijawahi kuwa kosa la jinai kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi. Amefafanua kuwa ikiwa kuna tuhuma nyingine dhidi yake bado kwa sheria za nchi alipaswa kufikishwa kwenye mamlaka za kisheria na si kuendelea kuzuiliwa.

“Natoa mwito kwa mamlaka kumwachia huru kwa sababu kuendelea kumshikilia ni kukiuka utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

TLS tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu suala hili na tutatoa msimamo wetu na mwelekeo baada ya mashauriano kufanyika kupitia baraza la uongozi," amesema Dk Hoseah.

No comments :

Post a Comment