airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 27, 2024

TUJIKUMBUSHE:BANDARI KONGWE YA PEMBA CHAKE MKOANI ILIJENGWA NA WAARABU TOKA GHUBA YA SHARJAH!

  • Asili ya wazanzibari ni ipi?
  • Watumbatu toka Taabuk
  • Wahadimu toka Ajemy
  • Wapemba toka Diba
:: Na Hussein Bashir Zanzibar/30 July/2023


Kwa mujibu wa Hollingsworth na Ingram katika kitabu Zanzibar it's people and Its history wanasema kuwa Waarabu waliingia Zanzibar miaka 200 kabla wabantu hawajakanyaga katika kisiwa hichi.

Hata hivyo wanazuoni wa historia wamekubaliana kuwa wenyeji wa wa Asili wa Zanzibar ni watumbatu, Wahadimu na wapemba

Ingawa zipo jamij kadhaa wa kadhaa ndani ya visiwa hivi vya marashi ya karafuu bila shaka jamii tulizozitaja ni miongoni mwa jamii za wenyeji wa Asili ya Zanzibar

Watumbatu wametoka katika mji wa Makkah na Taabuk

Asili ya watumbatu ni bara Arabu

Kulikuwa na makundi sita yaliyoingia mwambao wa Afrika mashariki toka bara Arab kundi la mwanzo lililingia mwambao wa Afrika ni hili kundi lililotoka katika mji wa Taabuk jirani kabisa na Mji wa Makka na kuingia katika visiwa hivi vya Tumbatu.

Kundi la pili lilitokana na banu Shuayb toka katika Mji wa Sirba(hili ni moja ya majina ya kale ya mji wa Makkah) kundi hilo liliingia Somalia,Lamu,Tanga mpaka Tumbatu

Makundi haya mawili yalikuja katika karne za mwanzo kabisa mpaka karne hii ya saba yaliendelea kutiririka.

Kundi la tatu ni kundi la kizazi cha Juni bin Qatada mmoja wa wafuasi wa Mtume Muhammad saw huko Madina kizazi chake kinafahamika kama wabaajuni

Hawa walikuja Afrika mashariki baada ya machafuko ya banu Umaya juu ya kadhia ya Sayyidna Ali ,kundi hili liliingia Somalia lakini pia lililazimika kuhama Somalia kutokana na vita vya Vutilo na Wakulo hivyo wabaajuni wakaingia Tumbatu

Kundi la nne liingia mwishoni mwa karne ya 7 na mwanzoni mwa karne ya 8 toka Yemen

Na kundi la tano ni lile lililotumwa na Abdulmalik Marwan khalifa wa kibanu Umayya aliomtuma mwanaye Hamza Ibn Abdul Malik Marwan kuja kufundisha ilmu ya Fiqhi hapa na kujenga miji ya Afrika mashariki miongoni mwa miji hiyo ni mji huu wa Tumbatu

Na katika kipindi hicho ndio ukajengwa msikiti wa Limbani Tumbatu Jongoe ambao ulijengwa mwa wa 36 hijiriya kama unavyojieleza katika maandishi yaliyoandika hapo msikitini kwa lugha ya kiswahili kutumia hati za kiarabu kuwa " Msikiti wa Limbani Tumbatu Jongoe umejengwa mwaka wa 36 Hijiriya na kuanza kutumika mwaka 37 Hijiriya

Kundi la sita ni kundi la wahamiaji toka Ajemy (washirazi) walioingia mwambao huu karne ya 9-12 katika kipindi hichi ndio aliingia Sultan Yusuf bin Alawy mtoto wa Mfalme wa Shirazi aliyetoka Bushire

Yeye aliujenga Msikiti wa ijumaa wa Tumbatu uitwao Masjid Jame na misikiti mengine minne sambamba na nyumba zaidi ya 380 kadhalika alijenga kasri yenye vyumba takriban iliyotazama Bahari ya Hindi , kasri hiyo ilikuwa na milingoti miwili ya bendera

Katika kipindi hichi cha ujio wa hawa washirazi ndio uliopelekea kujengwa Msikiti wa Kizimkazi ambao ndio kielelezo cha misikiti mikongwe hapa Zanzibar msikiti huu wa Kizimkazi ulijengwa mwaka 500 Hijiriya sawa na mwaka 1107 kama ulivyoandikwa kwa herufi za kikufi ndani ya Mihrabu ya Msikiti huu

Major peace katika kitabu chake " Zanzibar the island of Metropolis anaeleza kuwa washirazi ni miongoni mwa wakazi wa kale wa Zanzibar

Wahadimu sio watumwa ni washirazi wenye sharfu zao

Katika karne ya 16 wareno walipoingia Zanzibar na kuanzisha biashara za utumwa Mwinyimkuu wa Tumbatu ambaye ni mshirazi aliozaliwa katika kizazi hichi kilichotoka Saadani Bagamoyo ndio alioomba msaada Oman kwa Imamu Seif bin Murshid Al yaaroub kuja kuvunja utumwa huo,Kisha Mwinyi mkuu akawaomba wakishawaondoa wareno wa Oman wasiondoke Zanzibar wabaki hapa wakiilinda Zanzibar dhidi ya uvamizi wa wareno

Waomani walikubali kwa sharti moja tu nalo ni kwamba wapewe msaada na wausaidizi wa mambo yote muhimu wawapo hapa Zanzibar kama vile makaazi na mashamba

Na hiyo ikapelekea waitwe " Wahadimu" kwa kuwahudumia wageni wao na sio watumwa wao kama baadhi wanavyowaita kwa kuwakejeli washirazi hawa wenye sharfu zao kiongozi wao na uwenyeji waliowakaribisha wageni ,mtumwa hawezi kuwa na sifa hizi

Ndio utakuta Shekh Ali muhsin Barwan ndani ya kitabu chake kujenga na kubomolewa Zanzibar uk 203 anasema neno Hadimu limetokana na neno " Hadamal ubadiya" yaani wenye kuvunja utumwa Kisha anasema kuwa hawa ni washirazi waliochanganya Damu na watu kutoka Asia na Afrika, Wahadimu wa kale wanasura za ki Asia zaidi kuliko za ki Afrika.

Kwa mfano Mwinyi mkuu wa Tumbatu Hassan Ahmed mtoto wa Malkia Fatma bint Yusuf Al Alawy sura yake ni ya ki Asia zaidi kuliko mwanawe

Mwinyi mkuu ndio aliowakaribisha waoman Zanzibar naye akakubali kuhamia Dunga Bweni kumpisha Sayyid said katika kasri yake ya Forodhani

Mwinyi mkuu huyu alipendwa na watu wake hata kumtungia nyimbo za kuwabembelezea watoto inayosema

" Karatasi na kutuma , kwa mfalme Hassani,yenye kanzu ya matola, na fimbo henzirani, kwa makosa niliyokosa,nina muombezi kwani,

Muombezi wangu nyota na baraka Ramadhani"

Wahadimu hawa wamechangia pa kubwa katika mila na desturi za wazanzibari,ingawa wanazuoni wa historia wanatafautiana kuhusu lugha ya kihadimu kuwa ipo au haipo lakini wanakubaliana kuwa kihadimu ni moja ya lahaja za kiswahili kama vile neno " Moo" maana yake. ni " Mguu" neno hilo limetumika katika kiswahili cha kale kwa mfano akina mama walilitumia katika nyimbo za harusi

" Bwana anakula solo na manya nyama" bwana anakula solo na manya nyama*

Muoshe "Moo" bwana na maji ya zamzam muoshe " Moo" Bwana na maji ya zamzam

Hapo bwana hukoshwa miguu ndio hiyo " Moo" rejea kitabu cha Shekh Abdallah Swaleh Farsy "Masultan wa Zanzibar- historia ya Sultan Sayyid said kayaeleza haya

Lakini pia salaam ya kizazibari "Chei chei" na "shikamoo" ni salaamu ya ki Asia kwani wao wakimuona mtu mzima humuamkia kwa kumshika miguu naye mtu mzima humshika kichwa huyo anayemuamkia kuonesha amekubali heshima ile

Kadhalika mwinyi mkuu vile vile huamkiwa kwa kushikwa miguu ingawa ilibadilika kidogo badala ya kushikwa miguu hiyo ilitosha kumwambia tu " nashika miguu yako" yaani "Shikamoo" naye huitikia " Marhaba" ikimaanisha nimekubali heshima yako kwangu jambo hili mpaka hivi Sasa wa Asia wanalidumisha kama tuwaonavyo katika luninga zetu

Bahati tulionayo makundi haya wametuletea pia salamu yenye baraka kutoka kwa mungu nayo ni "Assalaam Alaykum"- Amani ya Allah iwe juu yako

Wapemba ni Wadiba toka Sharjah


Katika pemba ni moja ya visiwa vikongwe Sana vilivyokaliwa na wenyeji ambao ni Waarabu kabla wabantu hawajatia mguu kisiwani hapo kuanzia karne ya kwanza ya Nabii Suleyman, kwa mujibu wa Hollingsworth katika kitabu chake "a school history of Zanzibar anaonesha kuwa moja ya misafara ya watu wa Nabij Suleyman waliingia pemba ikiwa mahala pao pakufanyia ibada wakipaita "Muswala" hivi leo panafahamika kama "Misali"

Waarabu hao waliofika katika kisiwa hicho pamoja na misafara hiyo ilichangia uanzishwaji wa Bandari Kongwe ya Mkoani

Bandari ya pemba ilijengwa na Waarabu tangu karne ya tatu mpaka karne ya saba ilipopita misafara mbali mbali ya mahusiano ya kibiashara Kati ya watu wa mwambao na watu wa mashariki ya mbali na mashariki ya kati kadhalika ilipofika karne ya 12 ulipofika ujio Waarabu wengine

Waarabu hawa kutoka Sharjah waliimarisha Bandari ya Asili huko pemba iliyokamata nafasi katika mwambao wa Afrika Mashariki baada ya Bandari ya Kaole Bagamoyo ikifuatana na bandari hii ya Mkoani Pemba

ambapo Bandari hii iliimarishwa kuanzia karne ya 12 na Waarabu hawa kutoka Sharjah ingawa ilianza kujengwa na Waarabu waliotangulia tangu karne ya tatu

Ingawa kuanzia karne ya tatu mpaka karne ya saba misafara mingine kutoka mji wa Makka ilifika pemba,zipo simulizi za misafara ya maswahaba waliokuwa wakielekea Habeshi Ethiopia walipita eneo hili wakiifuata bahari hii ya Hindi wakati huo ikiitwa " Al Bahry Habashy" kama alivyoieleza Qassim bin Hawqal Al Qasim ndani ya kitabu chake " Suratul Ardhi" ( the shape of Earth) Tazama pia katika kitabu " the great history of Afrika" hivyo masahaba hao walipokosea njia waliingia katika kisiwa hicho na kuoneshwa njia ya kuingia Habsh

Wakati huo pemba ikifahamika kama "Qambalu" - Ras mkumbuu ndio utakuta hapo unapatikana msikiti uliojengwa karne ya saba ya Mtume saw

Kama anavyoeleza Shekh Ali Muhsin Al Barwan ndani ya kitabu chake kujenga na kubolewa Zanzibar, kuwa Msikiti huu ulijengwa karne ile ile ya saba wakati Mtume bado yupo hai

Ndio utakuta happ Qambalu - Ras mkumbuu kuna mji ambao leo hij umefunikwa na bahari wenye mabaki ya karne ya saba kama utafiti wa Aero Survey unavyoonesha lakini pia ufukweni mwa bahari hiyo kuna magofu ya kale ya karne ya 7 mpaka 9

Mbali na Waarabu hawa waliokuja mwanzo kabisa lakini pia kuanzia karne ya 9-12 misafara mingine kutoka Shirazi na Ghuba ya Uarabuni Sharjah iliingia Pemba

Waarabu hawa walifahamika kama wadiba

Kwa mujibu wa John Gray ndani ya kitabu chake anasema kuwa " Diba" inapatikana baina ya bara Arab na Bara Hindi na Afrika katika visiwa vya Meldev ambavyo vilifahamika kama "Diba"

Lakini Shekh Ali Muhsin Al Barwan anasema kuwa " Diba" ya kweli iliyokusudiwa kuwa ndio asili ya wapemba inapatikana katika Ghuba ya mpakani mwa Oman na Sharjah Emirates Arabs ambapo watu wake wana asili ya Yemen

Wadiba hawa ndio waliokuja kutawala pemba hususan Pujini ingawa pia wananasibishwa na washirazi kisha wakachanganya damu na watu mbali mbali wa visiwa vya karibu na Pemba ilivyofahamika kama " Jaziratul hadhraa" yaani kisiwa cha kijani kwa rutuba nzuri

Wapemba wamechanganya damu na watu wa Mombasa, Tanga, mafia na Mrima

Kiongozi wa kale wa wapemba hapo Pujini alifahamika kama Mkama ndume , tumefafanua Sana maana ya jina hili katika kitabu chetu ' Utukufu wa Zanzibar" huyu ni mmoja kati ya wadiba hawa jina lake halisi ni Muhammad Abdulrahman Al Dibawy.

Hapo Pujini alijenga karsri kubwa na misikiti kadha wa kadhaa ambapo inapatikana misikiti ya kuanzia karne ya kumi na mbili mpaka karne ya 15

Kisha likaingia tena kundi jengine la Waarabu kutoka Oman yaani kipindi cha utawala wa akina Sayyid said ambapo napo nayo kumbukumbu ya magofu ya misikiti ya Chwaka Tumbe na Chwaka Haruna ambapo unamisikiti ya karne ya 16 mpaka karne 18 napo kuna vichekesho vya wasimamizi wetu wa utalii kwa kubandika majina na visa vya kejeli misikiti hiyo hapo kuna " Msikiti wivu" na msikiti chooko" (choroko kiswahili cha bara)

No comments :

Post a Comment