dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 22, 2024

ZACADIA YAZUNGUMZIA UPATIKANAJI WA ZANZIBAR DIASPORA IDs!

Baada ya kufahamika kuwa Wana-Diaspora kutoka Zanzibar sasa washaanza kupata kadi maalumu ziitwazo ZAN DIASPORA IDs kutoka kitengo cha Diaspora, Ikulu, Zanzibar, blog hili lilimtafuta kwa uvumba na udi Vice-President wa Zacadia (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) nchini Canada Bw. Hassan Othman na kumuuliza faida ya kadi hizi na vipi kuzipata.

"Faida ni tele", alianza kutueleza Bw. Othman, "lakini faida moja kubwa zaidi ni kuwa sasa Mwana-Diaspora mwenye hii kadi au namba anaweza kununua asset yoyote Zanzibar yeye mwenyewe kwa jina lake bila ya kumtumia ndugu yake au jamaa yake, kama tulivyokuwa tukifanya huko nyuma", alitujulisha Bw. Othman.

Bw. Othman aliendelea kutufahamisha kuwa kuipata kadi au namba ya ID ni rahisi kama kwanza utajitengeneza kuvipata vielelezo vyote vinavyotakiwa.

"Ukitaka kujiandikisha kwanza kabisa inabidi uingie kwenye portal frame ya Zanzibar Diaspora:


Kabla hujaingia kwenye site unatakiwa ujitayarishe na vitu vifuatavyo:

[1] Passport yako ya Tanzania ya zamani
[2] Namba yako ya IF ambayo unaipata kwenye gamba la passport yako ya 
        zamani
[3] Jina lako kamili kwenye passport yako ya sasa (Current       
        Immigration Status)
[4] Next of kin:
Sasa hii NEXT OF KIN  inamasuala mengi. 
Next of kin anaweza kuwa baba, mama, mtoto, babu, bibi, etc.
Kuhusu next of kin inatakiwa uwe na haya yafuatayo:
[a] Jina lake kamili
[b] Tarehe yake ya kuzaliwa
[c] Uhusiano wenu ulivyo
[d] Contacts zake Zanzibar
[e] NIDA/ZAN ID namba yake
[f] Picha ya ID yake ya NIDA/ZAN ID/ Diaspora ID/ au Passport yake

Zaidi unatakiwa uwetayari na:
[5] Picha yako - passport size
[6] Picha ya passport yako ya nchi unayoishi
[7] Birth certificate yako 
[8] Police check kutoka mji unaokaa na mwisho uwe na
[8] Chochote kile chengine kinachoonesha kama wewe umehusiana na Zanzibar - yaani kama School Living Certificate ya Primary, Secondary au College au kitu chengine chochote kile.
Sasa ukesha kuvikusanya vitu vyote hivyo vya hapa juu ndio unaweza kuanza ku-apply kwenye website.

Ukeshaku-submit application yako haichukuwi muda utajibiwa kwa haraka sana kama umekubaliwa au unatakiwa upeleke vielelezo zaidi. Kama umekubaliwa unaletewa namba yako ya ID huku huku ughaibuni na kwa namba hii  unaweza kununa nyumba, ardhi, chochote kile japokuwa haupo Zanzibar, kupitia kitengo cha Diaspora kiliopo Ikulu, Zanzibar.

Ukifika Zanzibar mwaka wowote ule unakuenda Mazizini kwa ajili ya vipimo vya biometrics na unalipa Dollar 50 na unapewa kadi yako hapo hapo bila ya kuambiwa nenda na baadae urudi. Tunashukuru, so far kitengo kipo very efficient!
Hizi ndizo procedures za ku-apply", aliendelea Bw. Othman.

"Hatua ya mwanzo unapoingia kwenye site inabidi u-sign up na baadae wanakuletea password ambayo mara nyingi inaingia kwenye spam folder lako. Ukeshakuipata hii password inabidi u-login na ukesha ku-login inabidi uibadilishe ile password yao kwa password yako binafsi na baadae u-login tena ndio unaweza kuianza kazi yako.

Pakubabaika ni pale baada ya ku-sign up inafunguka page nyengine inakuambia weka email yako na password, lakini password hunayo - kumbe washakuletea na ipo kwenye spam folder lako. Kwahivyo, ukiwa careful kidogo hapa mwanzo basi kazi yako itakuwa rahisi sana," alimalizia Ndugu Othman.

Ndugu Othman pia alilijulisha blog hili kuwa yoyote yule anaeishi Canada anaweza kuwasiliana na Zacadia kama anataka msaada wowote ule katika kujaza hii form.
Contact details za Zacadia nchini Canada ni:
info@new.zacadia.com
Phone: 1.416.438.7857/416.994.6422/647.453.3856

No comments :

Post a Comment