dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 6, 2024

ZACADIA KUWASAIDIA WAPIGA MAKACHU WA FORODHANI, ZANZIBAR!

 MPIGA MAKACHU  ANAONEKANA AKIPIGA KACHU FORODHANI, MJINI ZANZIBAR!

Jumuia ya Diaspora ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada yenye makao makuu yake mjini Toronto, iitwayo ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association), imesema kuwa imo katika mipango ya kutaka kuwasaidia vijana wanaopiga makachu Forodhani, mjini Zanzibar, kwa kuwapatia ngazi 2 za stainless steel (SAE 316)/Aluminum (5052) ambazo zitawekwa kutoka baharini mpaka juu nchi kavu, ambazo watazitumia wapiga makachu hao badala ya  kuparamia sewage pipes zinazotoka Mji Mkongwe.

MPIGA MAKACHU WA FORODHANI AKIONESHA STYLE MPYA YA KUPIGA MAKACHU IJULIKANAYO KAMA FLATALA - YAANI UNAANGUKA KWENYE MAJI FLAT!

"Hawa vijana wanaifanya kazi nzuri kwa nchi yetu ya Zanzibar. Hakuna anaefika Zanzibar bila ya kufika Forodhani kuwaona. Tunazijua families zilizoakhirisha safari zao za kuondoka Zanzibar ili wapate muda wakuwaona hawa vijana wakipiga makachu na kwahivyo ni lazima tuyaboreshe mazingira ya huu mchezo wao, hasa kwavile sasa na akina dada pia wameanza kuonesha hamu ya kupiga makachu", alieleza Bw. Hassan Othman ambae ni Vice-President wa Jumuiya ya Zacadia nchini Canada.

"Sio kwamba hakuna ngazi ya kuendea juu, lakini zipo mbali kutoka pale wanapopiga makachu na kwahivyo vijana huamua kuparamia paipu za maji machafu kutoka Mji Mkongwe ili wafike juu haraka na kuendelea na mchezo wao", alifahamisha Bw. Othman.

SHIDA WANAYOIPATA HIVI SASA VIJANA WAPIGAO MAKACHU PALE FORODHANI NI KUPARAMIA MAPAIPU YA MAJI MACHAFU!

Alipoulizwa Bw. Othman kama tayari Zacadia ishawasiliana nao hawa vijana, Bw. Othman alijibu,"Hivi sasa tumo kuwatafuta na kutaka kujua vipi tutaweza kuwasaidia. Wenzetu ambao wapo mapumzikoni Zanzibar kwa muda huu wanaifanya kazi hio. Ni lazima tuwasiliane nao kwanza ili tujue kama wanaoushirika fulani au wanakutana kama marafiki tu jioni pale Forodhani. Bila ya wasiwasi, itabidi wapate kibali kutoka Baraza La Mji ili kupata ruhusa ya kuziweka hizo ngazi. Mamlaka ya Mji Mkongwe itabidi pia washirikishwe kwenye hatua yoyote ile", aliendelea Bw. Othman.

KUREJEA JUU BAADA YA  KUPIGA KACHU NI KAZI KWELI!

Alipoulizwa kipembeni Bw. Othman kama yeye ni mshabiki wa kupiga makachu au vipi, alijibu huku akicheka, "Kila baada ya miaka miwili huwa nakuenda nyumbani Zanzibar mapumzikoni na hukaa sio chini ya miezi miwili. Miezi miwili yote hii huimalizia Forodhani nikipiga makachu na vijana, kwahivyo naujua usumbufu wanaoupata vijana hivi sasa".

"Hizi kama zitakuwa portable ladders itakuwa vizuri sana - yaani wanazipachika pale wanapokuwepo wao wenyewe kwenye mchezo wao na wakiondoka wanazipachua na kuondoka nazo. Shida ni kuwa zitakuwa nzito. Zikijengewa permanently itakuwa ni vizuri zaidi, japokuwa tunaogopa kuwa wengine wasiohusika na huu mchezo wakaja kuzitumia  vibaya. Lakini, uamuzi wa mwisho utakuwa ni wao vijana", alitujulisha Bw. Othman.

AINA MOJA YA NGAZI AMBAYO ZACADIA INAFIKIRIA KUIWEKA FORODHANI 
KWAAJILI YA VIJANA WAPIGAO MAKACHU!

AINA YAPILI YA NGAZI ZACADIA INAFIKIRIA KUIWEKA FORODHANI  KWA WAPIGA MAKACHU!

"Email yetu Zacadia ni: info@new.zacadia.com na tunawaomba viongozi wa hawa vijana wawasiliane nasi", alimalizia Bw. Othman.



No comments :

Post a Comment