- KILA MWENYE MSIBA ANAKARIBISHWA KUKOSHA MAITI YAKE BURE!
- PIGA HODI NYUMBA YA NYUMA YA MSIKITI AU PIGA SIMU WAKATI WOWOTE: 0777.855.666; 0625.558.013; 0622.886.793;0778.767.070; 0655.953.103
Ijumaa ya tarehe 13 December, 2024, baada ya Sala ya Ijumaa, Msikiti wa Kwarara ukiwa chini ya uongozi wa Imaam wake, ulizindua chumba cha kisasa kilichojengwa kwa madhumuni ya kukoshea maiti.
Hichi chumba kinatoa nafasi ya utulivu kwa jamii katika kulinda utakatifu wa desturi za Kiislamu za kitamaduni.
Chumba hichi kimejaa teknolojia ya kisasa pamoja na vifaa vinavyohakikisha kwamba kazi ya kukosha maiti inafanyika kwa heshima na kwa hadhi kubwa.
Zipo zana maalum za usafi, mifumo ya maji inayofanya kazi kwa ufanisi na mifumo ya kudhibiti joto ili kudumisha mazingira mazuri wakati wa kukosha maiti.
Uongozi wa msikiti unatumaini kwamba maendeleo haya hayatasaidia tu katika kupata mazingira mazuri ya uhakika ya kukosha maiti bali pia kuipa jamii hisia za utulivu na amani ya akili wakati wa kipindi kigumu cha mtu kufiwa.

Zaidi ya hayo, msikiti unakusudia kutoa mafunzo kamili na kufanya semina kwa viongozi wa kidini kutoka jamii ya Kwarara na sehemu nyingine.
Lengo kuu ni kuhakikisha kwamba wanajamii wote wanajua taratibu sahihi na hivyo kuwawezesha kutoa huduma bora wakati wa msiba wa mmoja wao.
Mpango huu ulidhaminiwa na Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZACADIA) na unachukuliwa na wengi kama hatua muhimu ya kukuza umoja ndani ya jamii kwa kuwaleta wanajamii pamoja wakati wa msiba.
FOR THE ENGLISH VERSION OF THE ABOVE ARTICLE, CLICK THE LINK HERE BELOW:
No comments :
Post a Comment