Kwanza kabisa tunaomba kuwatoa hofu wale wenye dhana ya kwamba sisi tunakwenda Mahakama kuu kuishitaki serikali kali kwamba dhana Hiyo ni potofu. Sisi tunaenda mahakamani sio kupingana na serikali Bali kuomba Mahakama kutoa tafsiri ya vifungu kadhaa vya katiba pamoja na sheria ya uraia ya mwaka 1995.
Kuomba Mahakama kutoa tafsiri ya sheria za nchi ni haki ya kila mwananchi aliyeathirika na sheria hizo.
Pamoja na mapungufu mengi yaliyomo kwenye katiba yetu na sheria ya uraia ya mwaka 1995, tutaiomba mahakama kuu kuangalia mambo yafuatayo na kuyatolea tafsiri sahihi-
1)Katiba ya Tanzania ya mwaka 77 hailezei kinagaubaga tafsiri ya uTanzania.
Haisemi MTanzania ni Nani?
Hili linapekea kuwepo na matatizo mengi ya watu kusingiziwa uraia wa nchi zingine.
Mfano: Generali Ulimwengu, Zitto Kabwe na wengineo.
Kesi hii itaitaka mahakama kuitaka serikali Iweke bayana kwenye katiba tafsiri sahihi ya uTanzania na marekebisho ya katiba juu ya Jambo hilo.
2) Ibara ya Tano ya katiba ya JMT inaongelea haki ya kupiga kura. Kifungu cha pili cha ibara hiyo kinasema, nanukuu Sio word for word—“Katiba inalipa Bunge la JMT kuweka zuio la kupiga kura kwa MTanzania mwenye uraia zaidi ya nchi moja.
Katiba haisemi kinagaubaga juu ya kulipa mamlaka Bunge la JMT kumfutia raia wa Tanzania uraia wake pale atakapo chukua uraia wa nchi nyingine.
Tutaiomba mahakama kutoa tafsiri sahihi ya kifungu hiki cha katiba.
2) katiba ya Tanzania inazuia utengenezwaji wa sheria ndogo za kibaguzi. Everyone should be treated equally under the law. Lakini sheria ya uraia ya mwaka 1995 inawapa wanawake uraia pacha endapo wataolewa kwenye nchi zinazowapa wanawake hao uraia kwa kuolewa.
Hii ni sheria baguzi na hivyo kuifanya sheria ya uraia ya mwaka 1995 kuwa sheria batili.
3) kukosekana kwa due process kwenye suala la uraia. Katiba ya Tanzania inasema mtu hawezi kupoteza uraia wake bila ya due process. Lakini, citizenships Act ya mwaka 1995 inamnyang’anya MTanzania uraia wake automatically. Hii sheria inakinzana na matakwa ya kikatiba.
4: Citizenship Act ya 1995 inabagua watu walioa ama kuolewa na raia wa nchi nyingine kwa kuwapatia wanawake wali olewa na waTanzania wa kiume a pass to Citizenship na kuwanyima njia Hiyo wanaume waliooa wanawake wa kiTanzania.
Sheria Hii ina ubaguzi wa kijinsia kitu ambacho katiba yetu hairuhusu.
Kuna vifungu vingi vya sheria ya uraia ya mwaka 1995 vinavyokinzana na sheria mama (katiba).
Kwahiyo basi, hii kesi ina merit kubwa sana. Vilevile, tukishinda ama kushindwa kwa sababu za kisiasa tunaweza kuipeleka hii kesi kwenye mahakama ya East Afrika ama Mahakama ya Afrika kutafuta hukumu bora za kisheria.
Hatuwezi kuyafanya yote haya bila ya mchango wako Kama diaspora ama MTanzania yeyote. Please support us with any amount to put the lawyers at work.
Naamini tutashinda hii kesi.
kila mtu amwangalie mtoto wake usoni na amwambie nini anafanya kulinda utanzania wake.
Haijalishi Kama wewe una passport ya Tanzania ama la. Mtoto ama watoto wako wakitimiza miaka 18 watalazimishwa kuchagua uraia wao.
Hii Sio issue ya wale waliochukua uraia wa nje pekee yao. Inatuhusu sote.
Uzalendo na mapenzi kwa nchi yako ni vitendo.
Nawashukuru sana ambao wametimiza wajibu wao wa kuchangia.
This is a defining moment for you and me.
Kama rais Kikwete alivyowahi kusema huko nyumba, “diaspora ni wazuri sana kuongelea yasiowahusu.” Let us be serious about the issues affecting us all.
Tunawashukuruni nyote
Uongozi wa Mpito TFDC"
FOR MORE FACTS ON THE ISSUE CLICK THE FOLLOWING LINK:
No comments :
Post a Comment