MWANA-BLOG MAARAUFU ASHTUKA KWA KUIONA BENDERA YA TAIFA YAPEPEA NJIANI....
Mwana-blog Mjengwa akielekea kwenye shamba lake
la mihogo huko Iringa leo asubuhi
"Ndugu zangu,
Ni kweli, Watanzania tunaendekeza sana siasa za vyama na kuiasahau Tanzania yetu. Leo asubuhi sana niliianza safari yangu kutoa Msamvu , Morogoro kuja Iringa. Ni kawaida kando ya barabara kwenye makazi ya watu au vibanda vya biashara kukuta ikipepea, ama, bendera ya CCM, Chadema, CUF, Simba au Yanga. Lakini, ni nadra sana kuiona ikiperushwa bendera ya taifa letu.
Leo pale kijijini Mtandika, nje kidogo ya Ruaha Mbuyuni niliona kwenye banda moja la biashara ikipepea bendera ya taifa. Nilishtuka kuiona , niliguswa pia. Nlipunguza hata mwendo kumwangalia kijana yule aliyekuwa akifanya biashara yake ya vitunguu huku bendera ya nchi yake ikipepea.
Maana, bila shaka kijana yule kwa mapenzi ya nchi yake aliitafuta mwenyewe bendera ile ya taifa. Kwa vile, unapoona mahali kuna vijana wanapeperusha bendera za vyama yaweza kuwa na tafsiri ya ama, ni wapenzi wa vyama hivyo, na kuwa wamezitafuta wenyewe, au kuna kada wa chama husika aliyekuja na kugawa bendera hizo kwa vijana hao.
Ndio, tunahitaji kufanya jitihada za kuwafanya watu wetu waipende nchi yao waliyozaliwa, kutoka ndani ya mioyo yao. Na moja ya jitihada hizo ni kuwapa maarifa yatakayowawezesha kujitambua, kujiamini na kuthubutu.
Maggid,
Iringa.
0788 111 765".
No comments :
Post a Comment