*LEO TUNAMKUMBUKA"
The Late President of Tanzania - Mwalimu Julius Nyerere
Ni miaka imepita enzi za baiskeli mpaka sasa kuna Guta/
Njoo upesi baba uwaone wezi wanatupa suluba kimyakimya bila vita/
Ningekutajia majina sema tu moyo unasita.
Wale uliowaacha vijana sasa ni wazee mfano Samweli Sita.
Wale wabunge wako watiifu hawapo tena sasa kuna mafisadi/
Wanataifisha ardhi yako tena hasahasa migodi/
Kisha wanapewa heshma kwa kuchongewa jembe la Gold/
Tuliyemtegemea mtafanana kumbe naye goigoi/
Amekufanana jina tu ila kimatendo bora Toi/
Njoo maramoja baba uturejeshe kwa wakoloni/
Hapa kwenye uhuru tunaishi kama motoni/
Sera ya kujuana inawatesa wanazuoni/
Hata waliosoma sana ajira hivi sasa hawazioni/
Yule mwenye kitambi alituletea shule za kata/
Mwenzake amekuja hana jipya ujinga mtupu amepakata/
Heri tumpe faida mchuuzi tuvujishe hili pakacha/
Hawa wapinzani na watawala nao wanafanana kama mapacha/
Bunge lako tukufu sasa wanaimba kwasakwasa/
Wanapeana mipasho waziwazi wanadai hizo ni siasa/
Sheria zimebadilika sasa askari ruksa kufanya mauaji/
Thubutu kuwakemea nawe uende na maji/
Mgambo wa jiji kamgeuza machinga mtaji/
Ushoga na uchangudoa biashara halali katikati ya jiji/
*LEO TUNAMKUMBUKA"
(Mtunzi hajulikanwi)
No comments :
Post a Comment