dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 9, 2012

Umoja wa Wazanzibari Skandinavia wasema:

KUUNGA MKONO TAMKO LA PAMOJA
Written by   //  08/10/2012  //  Habari  //  1 Comment
Umoja wa Wazanzibari Skandinavia umepokea kwa furaha kubwa azimio rasmi lililotolewa na washiriki wa Kongamano la Kitaifa lililofanyika katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani tarehe 6 Oktoba. Wazanzibari Skandinavia inaunga mkono moja kwa moja juhudi zinazoendelea za kuwaungansiha Wazanzibari wote, bila ya kujali itikadi zao za vyama vya kisiasa na tafauti nyengine za kijamii.
Hii ni fursa adhimu kwa wananchi wote wa Zanzibar wanaopenda maendeleo, amani na demokrasia kujitokeza kwa wingi, na kutowa mawazo yao kwenye Tume ya Katiba, wakati huu Tume inapoendelea na mchakato wa kukusanya mawazo ya wananchi nchini Zanzibar, juu ya uundwaji wa katiba mpya ya Tanzania. Hadi sasa Wazanzibari wengi wameonesha haja yao ya kuwa na muungano wa MKATABA, kwani muungano uliopo sasa wa kikatiba umewaondolea imani ya kuweza kupata dola yao na UHURU wao wa kudumu.
Umoja wa Wazanzibari Skandinavia inaunga mkono hoja na haja ya kuwepo kwa katiba inayoendana na wakati na matakwa ya wananchi, na inayotamka wazi mamlaka ya Zanzibar (Zanzibar’s sovereignty). Kwa kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar imejengeka kutokana na ridhaa za wananchi, ni matarajio yetu kwamba serikali itachukuwa juhudi za makusudi kulinda haki za raia katika kutoa maoni yao bila ya vitisho na pingamizi zozote. Tunaamini kuwa serikali haitawavumilia wale wote wasioitakia mema Zanzibar, ambao wanatumia njia mbali mbali katika kuwafitinisha na kusababisha uhasama baina ya Wazanzibari.
Mwisho, ni imani yetu kwamba serikali itahakikisha kwamba Tume ya Katiba inasimama katika misingi ya ukweli, uwazi na uadilifu. Na kwamba itawasilisha bila ya ubabaifu mawazo na madai ya wananchi wa Zanzibar katika uundwaji wa katiba mpya na mustakbali wa Zanzibar na Wazanzibari.
Mungu ibariki Zanzibar,
Uwabariki Wazanzibari na viongozi wao. Amin
R.M.Rashid (Mwenyekiti)
Umoja wa Wazanzibari Skandinavia
Nørre Allé 7
2200 Copenhagen
Denmark
www.wazanzibariskandinavia.wordpress.com
Nakala:
• Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr. Ali Mohammed Shein
• Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
• Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi
• Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Pandu Ameir Kificho
• Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba

Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment