Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya michanga ya ardhi ya Zanzibar na Tanganyika wakati wa Muungano 1964 huku (kulia) aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Rashid Mfaume Kawawa akiangalia tukio hilo na nyuma (kushoto) aliyekuwa Rais wa Zanzibar Abeid Amani Karume akishuhudia tukio hilo.
WAULIZA WAZANZIBARI: JE, HILO LILIKUWA TUKIO
BAINA YA WAUNGWANA (WATANGANYIKA) NA
WATUMWA (WAZANZIBAR)???
(ONE STUPID PERSON NEEDS TO APOLOGIZE
IMMEDIATELY)
KITENDAWILI CHA NYERERE
Nyerere kama binadamu wa kawaida alikuwa na mapungufu yake ila naomba tuweke mizani ya mapungufu ya Nyerere na mazuri aliyotutendea. Nionavyo mimi walionufaika na makosa ya Nyerere ndiyo hao wanaomtukana leo kwa kutowatendea sawa. Kosa la kwanza la Mwalimu ni kupenda haki na usawa. Alitamani sana sisi sote tuishi sawa kama waishivyo wateule walioko peponi. Alitaka watu wote waelimike sawa na kwa kadiri ya juhudi ya mtu, ndiyo maana akanyang'anya shule za makanisa na kuzifanya kuwa za umma ili watu wote wasome bila kujali imani yao. hili ni kosa kubwa alilopata kulitenda kama angelijua hawa walionufaika na kosa hili wangemgeuka na kusema alikuwa anawapendelea wakristo. shule nyingi zilikuwa za Roman Catholic ambako ndiko imani yake katika kristo ililala.
Aliwakosea wakatoriki ili wale mapagani na wenye imani isiyosisitiza elimu dunia wasome. Aliona mbali kwamba wasome wa nchi hii wangekuwa wakatolic na waanglikana tu na waluteri wachache akawapa elimu kwa shule zilizotokana na sadaka za wakatoriki wala nguruwe. Mapagani na wale wengine wakaacha kujiita kina joseph, john, marko n.k wakawa wanasoma kwa majina yao ya asili wakiwa huru pasi kuulizwa hata dini zao. Kwa elimu waliyopata kupitia shule zilizojengwa na wakatoriki leo wanamkashifu mwalimu kwamba hakuwajali, (shukurani ya punda). Kosa la pili la Mwallimu ni kuiona Tanganyika ni moja na yeye kama Mtanganyika hakuwa na sababu ya kuipendelea Musona kwa namna yoyote ile, hivyo ikabaki nyuma kana kwamba hakuzaliwa huko. Hawa ambao miji yao ilipata maendeleo katika kipindi cha utawala wa mwalimu ndiyo wanaomkashifu leo.
Kosa lingine la mwalimu ni kupenda umoja hata akaiunganisha Tanganyika na kisiwa na watumwa na matokeo ya kosa hili tunayona wazi leo kupitia uamsho.
Kosa lingine la mwalimu ni kutokuwa na upendeleo kwa familia yake. Hadi anastaafu uraisi alikuwa na watoto wakubwa na wasomi wazuri tu lakini hakuwaachia hata uwaziri au ujumbe wa halmashauri kuu ya Chama alichokipigania. Kosa hili linawafanya watoto wa mwalimu kutokuwa na nguvu ndani ya chama cha baba yao. Ona wenzake wanavyokalia nafasi muhimu ndani ya chama wakishirikiana na watoto na wake zao. Kosa lingine la mwalimu ni kutokuwa mjasilia mali kwa kutumia rasilimai lukuki za taifa alizoziacha. Alijua kuna madini, gesi, mafuta, misitu na wanyama pori ambavyo vingeweza kumfanya awe tajiri kama Gadafi na Mabuut lakini akaaviacha mikoni mwa watu walafi ambao leo kwa utajiri walioupata kupitia rasilimali zetu wanamtukana mwalimu kwa kosa lake la kutopenda kuwa tajiri akiwa duniani labda alikuwa anajiwekea hazina mbinguni ndiyo maana wanapigania kwa nguvu zao zote atangazwe mwenye heri. Kosa lingine la mwalimu ni kutoa elimu ya bure kwa wote bila upendeleo kiasi kwamba hata watoto wa masikini wakasoma sawa na watoto wa watukufu/waheshimiwa na leo watoto wale wa masikini waliosoma bure kwa makosa ya mwalimu ndiyo wanaomtengenezea kashifa kila uchao. Kama angelijua angewaacha wakaishia kuwa wachunga ng'ombe na wakulima uchwara huko vijijini kwao wasingepata pa kumtukania mwalimu maana wangekuwa mbumbumbu. Kosa lingine la mwalimu ni kutoa matibabu bure na sawa kwa wote bila kutenga wa kutibiwa India na wale wakutibiwa kwenye dispensari zisizo na dawa huko vijijini. Kosa lingine la mwalimu ni kutoficha mabilioni ya fedha huko nje wakati nafasi alikuwa nayo kwa miaka 23, atamlaumu nani? lazima atukanwe na hawa wajanja wa leo. Natamani kuandika alichofanikiwa sikioni mtanisamehe kwani huu ndiyo mwisho wa upeo wangu.
Chanzo: Wanabidii Forum |
No comments :
Post a Comment