Picha mbali mbali za mizoga ya faru ambao ambao wameuwawa
kwa sumu na kuondolewa pembe
kwa sumu na kuondolewa pembe
By Goldentz.blogspot.com
Friday, Nov. 09, 2012.
Vifaru wanakabiliwa na tisho la kuwindwa kiharamu
Mahakama nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miaka arobaini raia mmoja wa Thailand aliyepatikana na hatia ya kuuza pembe za vifaru na kuandaa maonyesho ya uwindaji yasiyokubalika
Chumlong Lemtongthai alikiri kosa la kuwalipa makahaba kuweza kufanya maonyesho ya uwindaji wa vifaru.Pembe hizo ziliuzwa barani Asia ambako soko la pembe hizi ni kubwa sana kwani hutumiwa kama dawa.
Zaidi ya vifaru miatano wameuawa nchini humo na wawindaji haramu mwaka huu pekee.
Akitoa hukumu hiyo jaji alisema kuwa hataki wajukuu wake wakuwe bila kujionea vifaru nchii humo.
Tanzania bado tunapiga bla bla tu kwenye hili. Tunatakiwa kuiga mfano wa Afrika Kusini katika kukabiliana na uharamia katika mbuga zetu. Tunasikia tu watu wanakamatwa lakini hawatajwi kwa majina hata kusikia wamepewa hukumu kali kama fundisho. Tuige mfano wa Afriak Kusini kuwaonyesha hadharani ili wajukuu wetu wajue kuwa Tanzania haina faru tena kutokana na uharamia wa fulani bin fulani.


Kitoto cha faru kikiwa hakijui la kufanya baada ya mama yake
kuuwawa na maharamia kwa ajili ya pembe

Bango likimwonyesha haramia Chumlong Lemtongthai raiya
wa Thailand aliyehukumiwa miaka 40 kwa kuua faru.

Haramia Chumlong Lemtongthai akiwa mahakamani Afrika Kusini

baadhi ya pembe za faru zilizokamatwa
Haramia Chumlong Lemtongthai akiwa mahakamani na mawakili wake

Haramia Chumlong Lemtongthai
Source: GoldenTzblog

No comments :
Post a Comment