Makala hii inayokuja katika muundo wa barua yangu binafsi kwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ni matokeo ya kero mbalimbali zinazoikabili Zanzibar kwa sasa. Kero hizi ni kubwa na zina athari kubwa kwa taifa hili, na cha kushangaza si wabunge wala wawaikilishi wameziwasiliha kwako Maalim wala katika vikao vya baraza za kutunga sharia nchini.
Maalim Seif nakuandikia barua hii wewe kwa sababu maalum. Kwanza mimi si miongoni mwa wanachama wako wala wafuasi wa chama chako. Lakini hili halinyimi mimi fursa ya kukuandikia na kukueleza kero zinazotukabili sisi na taifa hili kwa ujumla kwa sababu wewe ni Kiongozi wangu na napaswa nikuheshimu na niheshimu nafasi na mchango wako kwa taifa hili. Nakuandikia wewe kwa sababu pia mada ninayokusudia kuandika inahusu Mazingira jambo ambalo ni moja kati ya kazi zako.
Maalim Seif, sina shaka una habari na taarifa kuwa hali ya Ongezeko la joto nchini imeanza kukithiri na kufurutu ada. Wakati mataifa yakikataa kusaini mkataba wa Kyoto wa kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na viwanda, nchi zao zinafaidika na hali ya hewa ya wastani na baridi kali kali huku sisi tukiendelea kuangamia kwa joto kali na kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari.
Maalim Seif, kama umewahi kupita kule Wingwi Koowe, Jangwani Micheweni, Tumbe kwa mwinyi Uziwa, Vualeni, Liko kuu, kwa papa Kinowe sehemu nyingi ambazo mabonde na mashamba ya mipunga yako karibu na bahari utaokuta kuwa hayalimiki tena kwa kuingiliwa ni maji ya bahari. Hii ni hasara kubwa kwa wakulima na wananchi wa visiwa hivi. Naamini Serikali inafanya juhudi ya kulitatua hili lakini kwa uoni wangu kinga ni bora kuliko tiba. Ninachoomba mambo yafutayo uyapatie ufumbuzi ili kupunguza athari ya uharibifu wa mazingira hapa nchini.
Kwanza, tunakuomba uliangalie upya suali la uletaji wa mali kachara (used), mali chakavu, na mali mbofumbofu hapa nchini zinazoingizwa zikiwa hazina tena kiwango na ambazo ni hatari kwa mazingira. Maalim Seif nchi yetu imegeuzwa kuwa jaa la mali chakavu, nyingi zao zikiwa hazina faida tena hata kama zitaonekana kufanya kazi na kuuzwa kwa unafuu. Mfano mzuri ni mafriji yanayotumia gesi ya Chloro floro carbon (CFC) na vitu vyote vyenye kutumia gesi ya aina hii ambayo ni hatari kwa mazingira. Pia vitu kama Tivii, wino wa printers, na makompyuta mabovu yanayoletwa kwa kiwango kikubwa hapa visiwani. Maalim bila kuoneana haya na huruma tunaomba utupatie ufumbuzi juu ya hili.
Pili, Maalim Seif suali la uingizaji wa magari yasiyo na kiwango umekithiri sana nchini kwa sasa. Gari ambazo hazina kiwango ama kwa kuchoka kiumri, au kwa kuwa huko kwao zilipata matatizo makubwa ambayo kutokana na sababu na sharia za huko kwao haizingeweza kutumika tena na kwa maana hio huuzwa kwetu na kuletwa zikatumika barabarani. Maalim Seif, naamini utakubaliana nami kuwa asilimia kubwa ya ajali za barabarani zinatokana pia na magari yenyewe kuwa hayana tena kiwango na sifa za kutembea barabarani.
Isitoshe Maalim Seif, utakubaliana nami kuwa gari nyingi kubwa na chakavu zinaongoza katika uchafuzi wa mazingira duniani. Hapa kwetu hatuna utamaduni wa kuchunguza ubora wa magari yaingizwayo. Tunapokea na kutumia kila gari au hata meli bila ya kujali athari zake. Kwa hili ipo haja ya kuweka mipaka ya umri maalum wa gari kuingizwa nchini kwa sasa. Wenzetu Kenya wameweka wazi kuwa gari iliyo zaidi ya umri wa miaka kumi tangu kuundwa kwake au kuanza kutumika haiwezi kuingizwa nchini. Na hili si baya iwapo tutajali usalama wa raia na mazingira yetu.
Isitoshe Maalim Seif, utakubaliana nami kuwa gari nyingi kubwa na chakavu zinaongoza katika uchafuzi wa mazingira duniani. Hapa kwetu hatuna utamaduni wa kuchunguza ubora wa magari yaingizwayo. Tunapokea na kutumia kila gari au hata meli bila ya kujali athari zake. Kwa hili ipo haja ya kuweka mipaka ya umri maalum wa gari kuingizwa nchini kwa sasa. Wenzetu Kenya wameweka wazi kuwa gari iliyo zaidi ya umri wa miaka kumi tangu kuundwa kwake au kuanza kutumika haiwezi kuingizwa nchini. Na hili si baya iwapo tutajali usalama wa raia na mazingira yetu.
Mwisho, Maalim Seif uchafuzi wa mazingira umesababsihwa na ujenzi holela wa miji yetu. Leo hii mitaro na maji machafu kila pahala. Mitaro yetu pia humwaga uchafu katika bahari na kusababisha uharibifu mkubwa wa mzingira. Athari tunaziona. Kwa hili napendekeza idara zinazohusika ziangalie upya kupunguza uharibifu huu sambamba na kupitisha sera za mipango miji. Pia utaratibu wa kusanisi taka (recycling) uanzishwe ili kupunguza mrundikano wa taka taka mitaani.
Nakutakia kazi njema.
Asante.
Nakutakia kazi njema.
Asante.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment