Karandika lililobeba mahabusu wengine likiwasili mahakamani hapo bila ya mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi |
Askari polisi wakiweka ulinzi kumziba mwenzao asipigwe picha leo |
Wanahabari wakiwa wamejipanga kwa picha wakisubiri mtuhumiwa kuletwa mahakamani hapo
SAKATA ya mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limeendelea kuchukua sura mpya mkoani Iringa baada ya askari polisi anayetuhumiwa kuhusika na mauwaji hayo kufichwa katika gari maalum na askari wenzao .
Tukio hilo lilitokea leo wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa mahakamani huku askari polisi hao muda wote walionekana kuzunguka huku na kule katika mahakama hiyo kama njia ya kuwathibiti wanahabari waliokuwepo mahakamani hapo wasipate nafasi ya kumpiga picha mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenzao mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23).
Hata hivyo kabla ya kuingia karandika la mahabusu wengine gari ya polisi aina ya Toyota yenye namba za usajili PT 1404 ikiwa na askari zaidi ya 10 ilifika katika viwanja hivyo vya mahakama na kuegeshwa pembeni bila ya mtuhumiwa huyo aliyekuwa amefunikwa sura yake kwa kofia na kufichwa kabisa sura yake kuonekana huku akiwa amekaa mbele kwa dereva huku akifichwa na askari mwenzake pasipo kushuka.
Hata hivyo kabla ya kuingia karandika la mahabusu wengine gari ya polisi aina ya Toyota yenye namba za usajili PT 1404 ikiwa na askari zaidi ya 10 ilifika katika viwanja hivyo vya mahakama na kuegeshwa pembeni bila ya mtuhumiwa huyo aliyekuwa amefunikwa sura yake kwa kofia na kufichwa kabisa sura yake kuonekana huku akiwa amekaa mbele kwa dereva huku akifichwa na askari mwenzake pasipo kushuka.
Zikiwa zimebaki kama dakika 10 mahakama kuanza gari hilo lilisogea hadi mlango wa Mahakama na askari waliokuwepo mahakamani hapo zaidi ya 20 kulizunguka gari hilo huku wengine wakiwathibiti wanahabari akiwemo mwandishi wa habari hizi kama njia ya kuzuia kupigwa picha kwa mtuhumiwa huyo. Baada ya kuingia ndani ya mahakama, kabla ya hakimu kufika uthibiti ndani ya chumba cha mahakama ulikuwa mkali zaidi dhidi ya wanahabari hasa wale wenye kamera.
Wakati huo huo Mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa imeahirisha kesi hiyo ya mauwaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi ambae pia alikuwa ni mwenyekiti klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC), mtuhumiwa huyo askari mwenye namba G2573 Simoni (23) atafikishwa tena mahakamani hapo Desemba 5 mwaka huu kesi hiyo itakapo tajwa tena.
Mwendesha mashitaka wa jamhuri Adolf Maganda aliieleza mnahakamani hiyo mbele ya hakimu Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.
Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.
Chanzo: WotePamoja
No comments :
Post a Comment