Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 30, 2012

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi atembelea makazi ya padri Ambrose Mkenda

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifuatana na Father Shayo wa Kanisa la Roman Katholic liliopo minara miwili     baada kuwafariji na kutoa mkono wa pole  kwa uongozi wa huo kufuatia kujeruhiwa kwa Paroko wa Parokia ya Mpendae Padre Ambrose Mkenda
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifuatana na Father Shayo wa Kanisa la Roman Katholic liliopo minara miwili baada kuwafariji na kutoa mkono wa pole kwa uongozi wa huo kufuatia kujeruhiwa kwa Paroko wa Parokia ya Mpendae Padre Ambrose Mkenda
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifika katika makazi ya padri Ambrose Mkenda  wa Paroko wa parokia ya kanisa katoliki la Mpendae Zanzibar kuupa pole uongozi wa Kanisa hilo pamoja na Familia yake kufuatia ajali ya  kupigwa risasi hivi karibuni na watu wasioujulikana…
Tukio hilo la kusikitisha lililofanywa na watu wawili waliopakiana kwenye Vespa lilitokea  langoni mwa Skuli ya Francis Maria iliyopo Tomondo Wilaya ya Magharibi ambapo ndio makaazi ya Padri Ambrose.
Balozi Seif akiufariji Uongozi huo alisema ni jambo baya na la kusikitisha lililofanywa na watu hao ambalo limetoa sura mbaya  kwa Taifa na Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo na haitasita kuwachukuliwa hatua za kisheria watu watakaobainika kufanya  uhalifu huo.
Alisema Serikali imesikitishwa na kulaani kitendo cha watu hao ambacho kinaashiria uvunjifu wa amani pamoja na kuwaweka wananachi katika hali ya wasi wasi usio wa lazima ndani ya harakati zao za kimaisha.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Uongozi na Familia ya Padre Ambrose Mkenda Kiongozi kutoka  Kanisa la Roman Katholic Father Shayo aliiomba Serikali kuendelea kuimarisha ulinzi wa raia wema ili kupunguza hofu iliyotanda mioyoni mwao kutokana na matukio ya uvamizi.
Father Shayo alitahadharisha kwamba hulka mbaya  iliyoanzishwa na baadhi ya watu kuwafundisha watoto wadogo tabia ya kukashifu watu wazima kwa sababu ya utofauti wa Kidini inawajengea maisha mabovu watoto hao.
“ Watoto wadogo kufundishwa tabia ya kukashifu watu wengine tuelewe kwamba Taifa halitakuwa na muelekeo mwema wa jamii yake ya baadaye”. Alitahadharisha Father Shayo.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment