dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 12, 2013

UCHAGUZI 2015: Aomba asichaguliwe asipotimiza ahadi


MBUNGE wa Jimbo la Iringa ,Mchungaji Peter Msigwa 
Na Geofrey Nyang’oro Iringa

Posted  Ijumaa,Januari11  2013
KWA UFUPI
“Ninajua kero ya maji na barabara ndizo zinazowatesa wakazi wa kijiji hiki hususani wakina mama, lakini niseme tu kwamba suala la maji, nimefurahi kuna mfuko mnaendelea kuuchangia deni lililobaki ninalimalizia sasa na kuhusu barabara tayari nimeshaleta greda nitahakikisha barabara hii inatengenezwa, nisipotimiza ahadi hizi msinipigie kura mwaka 2015,”
MBUNGE wa Jimbo la Iringa ,Mchungaji Peter Msigwa amewataka wakazi wa Kijiji cha Kigonzile, katika Manispaa ya Iringa kutomchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ikiwa hatatimiza ahadi ya kuwapelekea maji na barabara katika kipindi hiki cha uongozi wake.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kigonzile juzi, Msigwa alisema amepania kuwafikishia maji na barabara wakazi wa kijiji hicho ili kuwapunguzia kero ya kutafuta maji na adha ya usafiri.
“Ninajua kero ya maji na barabara ndizo zinazowatesa wakazi wa kijiji hiki hususani wakina mama, lakini niseme tu kwamba suala la maji, nimefurahi kuna mfuko mnaendelea kuuchangia deni lililobaki ninalimalizia sasa na kuhusu barabara tayari nimeshaleta greda nitahakikisha barabara hii inatengenezwa, nisipotimiza ahadi hizi msinipigie kura mwaka 2015,”alisema Msigwa.
Aliwataka wamhukumu kwa ahadi zake kwani atayafanya hayo katika kipindi cha miaka miwili.
Katika mkutano huo, Msigwa alitoa Sh1.06 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji unaotekelezwa kwa ubia na wananchi pamoja na Serikali kwa msaada kutoka Benki ya Dunia.
Katika mradi huo wananchi walitakiwa kuchanga Sh3 milioni ambapo hadi mbunge anakwenda kufanya mkutano juzi walikuwa wamechanga Sh1.04 milioni .
Mwenyekiti wa kamati ya maji wa kijiji hicho, Emsy Silla alisema fedha zilitakiwa kuchangiwa na wananchi ni Sh3 milioni ambapo zingechanganywa na michango mingine kutoka Benki ya Dunia na Serikali ya Manispaa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Katika mkutano huo wakazi wa kijiji hicho walilalamikia kukosekana kwa huduma mbalimbali za kijamii katika kijiji chao ikiwamo huduma za afya na maji safi na salama wakidai hali hiyo inahatarisha maisha yao.
Akijibu hoja hizo mbunge huyo alisema suala la kukosekana kwa huduma ni tatizo la kitaifa na kwamba limekuwa likilalamikiwa katika maeneo yote nchini lakini akasisitiza uchache wa idadi ya wabunge wa chama chake unachangia kupitishwa bajeti isiyokidhi huduma za afya.
Chanzo: Mwananchi

No comments :

Post a Comment