Written by Wa Wawi // 23/01/2013
Waziri mkuu wa Uingerza Bw. David Cameroun amewaahidi raiya wa Uingereza kuwa ataitisha kura ya maoni ya wananchi ili kujua ikiwa wanataka kuendelea kuwemo katika muungano wa ulaya au la pindipo akichaguliwa tena kuliongoza tena taifa hilo mwaka 2015.
” sasa ni muda muafaka kwa wananchi wa uingereza kusikia kauli yao. Ni muda wetu wa kuamua juu a suala hili la (Nchi yetu ) Uingerza kuwemo katika muungano wa Ulaya au la” alisema waziri mkuu Cameroun”
“wakati tutakapojadiliana juu ya mambo kadhaa mapya ya umuhimu, tutawapa raiya wa Uingereza nafasi ya kupiga kura ya maoni yenye suala jepesi na la moja kwa moja la ikiwa wanataka kuendelea kuwemo kwenye muungano wa Ulaya kwa kuzingatia kanuni mpya au wanataka kujiondoa moja kwa moja.” aliongeza waziri huyo
hata hivyo kauli hiyo ya cameroun imeoneka kuishughulisha sana marekani ambaye ni rafiki wake wa karibu. Marekani inataka Uingerza indelee kubakia katika Umoja wa Ulaya ikiwa na sauti zaidi.
Chanzo: Aljazeera
No comments :
Post a Comment