
Hayati Baba wa Taifa.
Na Abdallah Bakari, Mtwara
Posted Ijumaa,Januari11 2013.
Posted Ijumaa,Januari11 2013.
Kwa ufupi: “Sio mimi ni Mwalimu Nyerere anasema….wengi katika nchi zetu ni wajinga ndiyo maana wanakubali kutawaliwa hivyo, kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ya ujinga tu, hivyo basi Watanzania watakuwa wajinga na mataahira (idiots) kama watakubali kuendelea kukandamizwa na kikundi cha wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe”.Katibu huyo alisema Nyerere katika kitabu hicho anasema“
Katika mkutano mkubwa uliofanyika jana Mtaa wa Sinani mjini hapa viongozi wa CUFWilaya ya Mtwara Mjini, walikuja na mbinu mpya ya kuhamsisha wananchi kuendelea na msimamo huo kwa kutoa hotuba za nukuu ya kauli za Baba wa Taifa kuhusu mustakabali wa hali ya maisha ya wananchi katika mazingira ya wachache kuwakandamiza wengi.
Saidi Kulaga, Katibu wa CUF Wilaya ya Mtwara mjini alisema kinachotokea leo kwa wakazi wa mikoa ya Kusini ni kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye kwa nyakati tofauti alinukuliwa akionya viongozi kuandamiza wengi.
Katibu huyo akisoma karatasi ya nukuu hizo kutoka katika kitabu cha ‘Reflection on Leadership in Africa’ kilichopigwa chapa na VUB University Press, 2000 alisema mwasisi huyo wa Taifa katika kitabu hicho amenukuliwa akisema
“Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala, mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wanapoteza matumaini na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?”
Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu Kulaga alisema “Sio mimi ni Mwalimu Nyerere anasema….wengi katika nchi zetu ni wajinga ndiyo maana wanakubali kutawaliwa hivyo, kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ya ujinga tu, hivyo basi Watanzania watakuwa wajinga na mataahira (idiots) kama watakubali kuendelea kukandamizwa na kikundi cha wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe”.Katibu huyo alisema Nyerere katika kitabu hicho anasema“Ni ukweli usiopingika kuwa masuala ya maendeleo hayawezi kuwa masuala ya ubabaishaji tu na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku chache zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao (wananchi) na watoto wao wakiendelea kuishi maisha duni na dhalili”.
Alibainisha kuwa kwa kuwa Serikali imeshindwa kuyaenzi maneno ya Mwalimu Nyerere wakazi wa Mtwara wamejitolea kuyaenzi maneno hayo kwa vitendo na kwamba hakuna tone la gesi ghafi litakalosafirishwa kwa njia ya bomba hadi Dar es Salaam.
Alifafanua kuwa wananchi wanatambua wazi kuwa gesi ni rasilimali ya Taifa lakini alihoji kwa nini Twiga wanaopatikana katika hifadhi za Serengeti hawahamishiwi katika hifadhi za kusini ilhali ni rasilimali ya Taifa?
“Naomba Tueleweke hatupingi gesi kunufaisha Taifa ila tunapinga mitambo ya kufua umeme kujengwa Dar es Salaam , tunataka mitambo na viwanda vijengwe Mtwara halafu faida itakayopatikana ilinufaishe taifa” alifafanua Kulaga
Katibu huyo pia aliweka hotuba ya Nyerere mkutanoni hapo inayopinga matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa kunufaisha wachache huku wengi wakiendelea kuteseka, kitendo hicho kilivuta hisia za wengi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Cuf Taifa, Katani Katani alisema uvumilivu wa watu wa kusini wa kudhulumiwa fursa za maendeleo umefika mwisho na kwamba hawako tayari kuona gesi asilia ambaye alilifananisha kama karata ya mwisho ikishindwa kuwakomboa.
“Tushikamane kwa hili, tuweke tofauti zetu kando…tuiambie Serikali katika hili hapana…kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya salamu za mwaka mpya amesema lazima gesi itaondoka basi tunamweleza haiondoki ajiandae kwa hatua nyingine,” alisema Katani huku akishangiliwa na vijana.
Chanzo: Mzalendo
Mimi kama mwanamtwara nafarijika si kwa kupinga gesi kwenda Dar tu bali kwa kujitambua. Hii inaonyesha jinsi gani sasa tunaweza kuwa na maamuzi chanya katika kutetea haki zetu ambazo zilikuwa zikielea elea angani na mwisho kupotelea mikononi mwa mabepari kwa kukubali kuuza mali zetu kwa fulana na kipande cha KHANGA. Bila shaka wakati umefika wa kusema YATOSHA...KUBURUZWA SASA BASI.
ReplyDelete