
RAIS Jakaya Kikwete
Na Mwandishi Wetu
Posted Jumanne,Januari15 2013.
Posted Jumanne,Januari15 2013.
KWA UFUPI
Rais Kikwete alisema kuwa pamoja na uhusiano huo mzuri, nchi inakabiliwa na changamoto ya mgogoro wa mpaka wake na Malawi katika Ziwa Nyasa, ambao hata
RAIS Jakaya Kikwete amewaeleza mabalozi wa nchi mbalimbali kwamba Tanzania ni nchi salama, pamoja na changamoto mbalimbali zinazoendelea.
Rais Kikwete alisema jana kwamba kutokana na amani na uimara wa usalama uliopo, anajivunia pia ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania, majirani zake na mataifa mengine duniani.
Rais Kikwete alisema jana kwamba kutokana na amani na uimara wa usalama uliopo, anajivunia pia ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania, majirani zake na mataifa mengine duniani.
Rais Kikwete alisema kuwa pamoja na uhusiano huo mzuri, nchi inakabiliwa na changamoto ya mgogoro wa mpaka wake na Malawi katika Ziwa Nyasa, ambao hata hivyo kwa sasa unashughulikiwa katika ngazi ya juu ya usuluhishi.
“Ni matarajio yangu kwamba suala hili litapatiwa ufumbuzi wa kudumu na ninawahakikishia Tanzania imenuia kuona suala hili linapatiwa mwafaka katika mazingira rafiki na ujirani mwema,” alisema.Aliwaeleza mabalozi hao katika tafrija maalum iliyofanyika Ikulu jana kwamba mwaka jana ulimalizika kwa mafanikio baada ya thamani ya Shilingi ya Tanzania kupanda ikilinganishwa na mwaka juzi huku mfumuko wa bei ukishuka kutoka asilimia 19.8 hadi 12.1.
Mambo mengine aliyozungumzia Rais Kikwete katika tafrija hiyo ni Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Chanzo: Mwananchi
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1666022/-/11r461a/-/index.html
.
No comments :
Post a Comment