Written by ibnially // 02/01/2013
Mjumbe wa baraza kuu Taifa CUF ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Mh Ismail Jussa amesema kuwa Nchi yetu ya Zanzibar katika mwaka uliopita wa 2012 imefikia hatuwa muhimu sana iliokuwa inasubiriwa kwa kipindi cha muda mrefu kwani imewawezesha wananchi wake kutoa maoni yao juu ya muundo gaini wa Muungano wanaoutaka ndani ya nchi yao kati yake na Tanganyika.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumzana wafuasi wa chama cha wananchi cuf pamoja na wananchi mbali mbali katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya jana katika uwanja wa mzushi uliopo jimbo la mtoni wilaya ya Mjini Unguja, Mh Jussa amesema kuwa Wananchi wa Zanzibar kudai mamlaka ya nchi yao sio suala la uhizbu kama wananavosema baadhi ya watu wengine isipokuwa ni haki yao ya msingi kwani kutaiwezesha nchi yao kuwa na mamlaka kamili ambapo kutawapelekea kujiamulia wanachokitaka juu ya nchi yao hivo basi baadhi ya watu wanaosema kuwa kudai mamlaka kamili ni uhizbu wanakosea na hawapaswi kusema hivo.Akibainisha kuhusu mambo yalioikandamiza Zanzibar ndani ya Muungano huu uliopo hivi sasa ni pamoja na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuyachukua mambo yasikuwa ya Muungano kuyafanya kua ni ya Muungano jambo ambalo limedumaza nchi yetu kiuchumi zaidi na kuonekana kuwa ni nchi maskini sana dunian,i akibainisha mambo hayo yalioingizwa kinyemela ndani ya Muungano huo kuwa ni Masuala ya Sarafu suala hilo hapo awali halikuwemo kabisa ndani ya orodha hio na wakati lilipoingizwa hata Serikali ya Zanzibar haikuwa na Taarifa na walikataa kabisa kuingizwa kwa jambo hilo kwani mpaka kitabu kiliandikwa kwa kuonesha kutokuridhika kwao na kitendo hicho.
Sambamba na hayo Jussa ameleza kuwa Zannzibar ni miongoni mwa Nchi za Visiwa kama zilivo nchi nyengine Duniani hivo basi kwa kawaida Nchi za kisiwa hutegemea zaidi uchumi wake kutokana na Bahari pamoja na utalii lakini hali haipo hivo kwa Zanzibar kwani upande wa pili wa Muungano huu umehodhi mamlaka ya bandari ndani ya Zanzibar pamoja na suala Zima la Utalii kwani hata ukienda huko kwenye Ofisi za Balozi za Tanzania Nje ya nchi wanaitangaza Tanzania kiutalii na sio Zanzibar jambo ambalo ni miongoni mwa sababu zakuikandamiza Zanzibar kwa makusudi.
Aidha mh Jussa ameleza kuwa kuhusu suala la elimu Nchi yetu inakandamizwa sana ni hivi karibuni tu kila mtu kati yetu aliona wazi wazi kuwa Wizara ya Elimu ya Tanzania ilishawazuia wanafunzi wa Zanzibar kutokufanya Mitihani ya Taifa.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment