Na Mwinyi Sadallah
12th January 2013
Meli kubwa ya mafunzo ya ubaharia inatarajia kuwasili Zanzibar leo baada ya kukamilisha taratibu za uwekezaji wa mradi huo.Uchunguzi wa NIPASHE Jumamosi umebaini kuwa meli hiyo inamilikiwa na Kampuni ya Philtex Limited ya nchini Dubai na tayari watendaji wa Kampuni hiyo wamewasili Zanzibar kukamilisha taratibu za uwekezaji kitega uchumi Zanzibar.
Kampuni ya Philtex ina mkataba wa miaka 10 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa (SMZ) uwakala wa kusajili meli za kigeni zikiwamo za mafuta nchini humo.
Chuo hicho kitatambulika kwa jina la Chuo cha Ubaharia Zanzibar (ZIMS) na kitaanza kutoa mafunzo kwa wanafunzi zaidi ya 40 wakiwa ndani ya meli hiyo.
Chuo hicho kitatambulika kwa jina la Chuo cha Ubaharia Zanzibar (ZIMS) na kitaanza kutoa mafunzo kwa wanafunzi zaidi ya 40 wakiwa ndani ya meli hiyo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya usafiri baharini (ZMA), Abdi Omar Maalim, amethibitisha kuwa wawekezaji hao wamefika Zanzibar kwa malengo ya kuanzisha kitega uchumi hicho.
Hata hivyo, alisema kwamba ni mapema kuzungumzia mradi huo kwa kuwa wawekezaji hao ndiyo kwanza wanakutana na Kitengo cha Uwekezaji Vitega uchumi Zanzibar (ZIPA).
Hata hivyo, alisema kwamba ni mapema kuzungumzia mradi huo kwa kuwa wawekezaji hao ndiyo kwanza wanakutana na Kitengo cha Uwekezaji Vitega uchumi Zanzibar (ZIPA).
Uchunguzi wa NIPASHE umebaini kuwa meli hiyo ina urefu wa mita 94 ikiwa na uwezo wa kuchukua watu 54 wakiwamo wanafunzi 40.
Meli hiyo imetegenezwa mwaka 1976 nchini Poland na kufanyiwa matengenezo makubwa mwaka 1996 nchini Afrika ya Kusini.
Aidha meli hiyo ina jenereta sita zenye uwezo wa kuzalisha megawati tano za umeme pia ina vifaa vyenye uwezo kuona kitu kilichozama Bahari Kuu umbali wa mita 200 kutoka usawa wa bahari.
Meli hiyo ina mtambo maalum wa kurekodi matukio kwa picha za video (CCTV) na mfumo wa kuhifadhi takataka zinazotokana na meli hiyo yakiwemo mafuta machafu.
Mradi huo iwapo utasajiliwa na ZIPA wanafunzi wataanza kusoma ndani ya meli kabla ya wawekezaji hao kujenga majengo yao visiwani Zanzibar.
Kabla ya kujitokeza wawekezaji hao wanafunzi wa ubaharia Zanzibar walikuwa wakisoma Tanzania bara au nje ya nchi.
Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Dk. Juma Malik alipoulizwa kuhusu mradi huo jana alisema hayupo katika mazingira mazuri ya kuzungumzia mradi huo.
Meli hiyo ina uwezo wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi 40 kwa wakati mmoja wakipata mafunzo ya vitendo na nadharia ndani ya meli hiyo.
Meli hiyo ina uwezo wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi 40 kwa wakati mmoja wakipata mafunzo ya vitendo na nadharia ndani ya meli hiyo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment