Posted on

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,(kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahaya Mzee,na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui
Na Salma Said
Mtakumbuka kuwa miongoni mwa malengo ya Mkutano wa sita wa Baraza la Biashara la Zanzibar, ilikuwa ni kushajihisha namna bora zaidi ya kuimarisha ushirikiano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi katika kuiendeleza Zanzibar na kuwaletea maendeleo wananchi wetu. Hili ni jambo moja ambalo wajumbe wa Mkutano huu wanaweza kulitathmini ndani ya kipindi hiki cha mwaka mmoja uliopita pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji na agenda yengine ambazo kwa pamoja tutazijadili na wahusika watazitolea ufafanuzi.
HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA
MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI,
MHESHIMIWA DK. ALI MOHAMED SHEIN,
KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA SABA WA
BARAZA LA BIASHARA LA ZANZIBAR (ZBC),
HOTELI YA BWAWANI – TAREHE 19 JANUARI, 2013.
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi,MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI,
MHESHIMIWA DK. ALI MOHAMED SHEIN,
KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA SABA WA
BARAZA LA BIASHARA LA ZANZIBAR (ZBC),
HOTELI YA BWAWANI – TAREHE 19 JANUARI, 2013.
Makamu wa Pili wa Rais;
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho,
Spika wa Baraza la Wawakilishi;
Spika wa Baraza la Wawakilishi;
Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania;
Dk. Abdulhamid Yahya Mzee,
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Baraza la Biashara la Zanzibar;

Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi;
Ndugu Wajumbe wa Baraza la Biashara la Zanzibar;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Assalaam Alaykum,
Awali ya yote naanza kwa kumshukuru Mola wetu Subhana Wataala; Muweza wa kila kitu kwa kutujaalia uzima na uhai tukaweza kukutana hivi leo katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar; tukiwa katika hali ya amani na utulivu.
Kwa hakika hii ni neema kubwa kutoka kwa Mola wetu kwa vile Mkutano huu unafanyika baada ya zaidi ya mwaka mmoja kupita, kwani matukio mengi yamepita katika kipindi hicho lakini kwa mapenzi Yake kwetu sisi bado tuko hai na tupo hapa kwa ajili ya kupanga na kuendeleza shughuli zetu za maendeleo.
Ndugu Wajumbe na Wageni Waalikwa,
Nachukua fursa hii kukukaribisheni na kukushukuruni nyote kwa kuitikia mwaliko wetu na kuhudhuria kwa wingi. Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wageni wetu nyote mliotoka nje ya Zanzibar.

Natoa shukurani maalum kwa ndugu zetu wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TNBC) kwa kuja kushirikiana nasi katika mkutano wetu wa leo. Kuwepo kwenu ni kielelezo cha ushirikiano mzuri uliopo baina yetu katika utekelezaji wa majukumu yetu. Napenda kukuhakikishieni kuwa tunauthamini sana mchango wenu na tunaendeleza ushirikiano huo kwa manufaa ya pande zote mbili na ustawi wa uchumi wa Tanzania.
Aidha, nina wajibu wa kutoa shukurani kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Baraza la Biashara la Zanzibar, ikiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa kazi nzuri wanayoifanya pamoja na maandalizi mazuri ya Mkutano huu wa leo. Vile vile, napenda kutoa shukurani kwa wajumbe nyote wa Baraza kwa ushirikiano mliotoa ndani ya kipindi cha mwaka mzima na mahudhurio yenu makubwa katika Mkutano wetu huu wa saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar. Nasema ahsanteni na karibuni nyote.
Ndugu Wajumbe na Wageni Waalikwa,
Huu ni Mkutano wa saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, ikiwa ni Mkutano wa pili tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa. Naamini kuwa ndani ya kipindi hiki tayari tumepata uzoefu wa namna bora zaidi ya kuendesha shughuli zetu kwa ufanisi kutokana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa, sambamba na kuimarisha uhusiano kati ya Serikali na sekta binafsi.
Huu ni Mkutano wa saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, ikiwa ni Mkutano wa pili tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa. Naamini kuwa ndani ya kipindi hiki tayari tumepata uzoefu wa namna bora zaidi ya kuendesha shughuli zetu kwa ufanisi kutokana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa, sambamba na kuimarisha uhusiano kati ya Serikali na sekta binafsi.
Mtakumbuka kuwa miongoni mwa malengo ya Mkutano wa sita wa Baraza la Biashara la Zanzibar, ilikuwa ni kushajihisha namna bora zaidi ya kuimarisha ushirikiano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi katika kuiendeleza Zanzibar na kuwaletea maendeleo wananchi wetu. Hili ni jambo moja ambalo wajumbe wa Mkutano huu wanaweza kulitathmini ndani ya kipindi hiki cha mwaka mmoja uliopita pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji na agenda yengine ambazo kwa pamoja tutazijadili na wahusika watazitolea ufafanuzi.
Ndugu Wajumbe na Wageni Waalikwa,
Katika mkutano uliopita, nilieleza lengo la Serikali la kuufanya utalii wetu uwe na manufaa kwa wananchi wote katika dhana ya “utalii kwa wote”. Napata faraja kuona kuwa wananchi wameufahamu vizuri umuhimu wa utalii kwa maendeleo ya nchi yetu kiuchumi na kijamii na kwamba tutaendelea kuongeza jitihada ya kuwafahamisha zaidi. Aidha, uwekezaji katika ujenzi wa mikahawa na mahoteli ya daraja mbali mbali ya kuwahudumia watalii umeongezeka. Hata hivyo, bado kuna haja ya kuimarisha ushiriki wetu katika shughuli mbali mbali za utalii pamoja na kuimarisha utalii wa ndani, kwani bado hatujaupa umuhimu unaostahiki. Nataka kukuhakikisheni kuwa Kamisheni yetu ya Utalii yutaendelea kuipa nguvu ili iweze kufanya kazi kwa kasi zaidi.

Mkutano wetu huu ni hatua muhimu katika utekelezaji wa azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuishirikisha sekta binafsi katika kuimarisha uchumi wa nchi yetu na ustawi wa wananchi kwa kuzingatia rasilimali tulizonazo na mipango yetu ya maendeleo endelevu. Katika Mkutano huu wa saba tumekuja na maudhui ya “Ubia na Uwekezaji kwa Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar” . Maudhui haya ndiyo yaliyopelekea kuchaguliwa mada kuu zitakazowasilishwa kwenye kikao chetu hiki cha siku moja ambapo mtapata fursa ya kuzichangia kwa kina.

Nina imani kuwa sote tunakubaliana kuwa viwanda vina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu na kuwapunguzia changamoto ya ajira kwa wananchi wetu. Katika hotuba yangu kwenye maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, nilieleza msimamo wa Serikali kuwa inatambua umuhimu wa kuwa na viwanda ili kuongeza vyanzo vyetu vya mapato, ambapo kwa mwaka wa fedha 2011/2012 mchango wake katika Pato la Taifa la viwanda ulifikia asilimia 3.9. Kwa hivyo, nilisema kuwa Serikali inaendelea kujenga mazingira mazuri yatakayopelekea kuvifufua na kuvikuza viwanda hasa viwanda vidogo vidogo, ili viweze kutoa mchango katika soko la ajira na kuinua mchango wake katika Pato la Taifa.
Ndugu Wajumbe na Wageni Waalikwa,
Napenda kukujulisheni kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuiimarisha sekta ya viwanda na jitihada za kuitekeleza dhamira hii zimeshaanza, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwepo kwa huduma za umeme wa uhakika, kuimarisha miundombinu ya barabara, bandari, uwanja wa ndege na sekta ya mawasiliano ya habari. Vile vile, washirika wetu wa sekta binafsi na wao watashirikishwa ili watoe michango yao, uzoefu wao na hatimae kueleza matarajio yao katika kulifanikisha jambo hili. Napenda kusisitiza umuhimu wa mchango wa sekta binafsi katika kufanikisha suala zima la maendeleo ya viwanda hapa nchini.

Nina matumaini makubwa kwamba baada ya Mkutano huu sote tutaamini kuwa nchi yetu ina fursa nyingi za uwekezaji katika viwanda vya aina mbali mbali, vikiwemo vinavyotumia mazao ya kilimo, mazao ya baharini na malighafi nyenginezo. Tuna fursa kubwa ya mazao yetu kuyaongezea thamani ili, tupate faida zaidi. Kwa hivyo, kwa mara nyengine nakutakeni nyote mtoe michango yenu kwa uwazi na bila ya khofu na baadae tutaondoka hapa na maazimio, ambapo kila mmoja wetu ataweza kutekeleza kwa mujibu wa nafasi yake.
Ndugu Wajumbe na Wageni Waalikwa,
Napenda kukuhakikishieni kuwa kila mtu yuko huru kuchangia maoni yake kwa kuzingatia utaratibu. Kama kawaida yetu tutakuwa wawazi katika kutoa ufafanuzi katika hoja zitakazohitaji maelezo ya ziada. Michango ya kila mmoja wetu ni muhimu sana katika kuyafanikisha Mkutano huu, na nakuhakikishieni kuwa tutaithamini na kuifanyia kazi kwa lengo la kuyafanikisha majukumu ya Baraza la Biashara la Zanzibar.

Baada ya kusema hayo, napenda nitamke kuwa Mkutano wetu wa saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar umefunguliwa rasmi na sasa tuendelee na agenda yetu.
Ahsanteni sana.

No comments :
Post a Comment