Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 22, 2013

MUUNGANO NI MAREHEMU!


WATANGANYIKA WAELEKEA UKINGONI BAADA YA KUITAWALA ZANZIBAR KWA MIAKA 49 KWA MWAMVULI WA MUUNGANO
Written by   //  21/01/2013
Kutokana na Darubini yetu ya kuangalia hapa na pale na kusikiliza maoni na maelezo ya Viongozi waliotangulia Zanzibar ”   Mh. Rais mstaafu Salmin Amour, Mh. na Mzee wetu Nassor Hassan Moyo, Mh. Rais mstaafu Amani Abeid Karume na wengine ambao darubiri yetu haitoweza kuwamaliza bila ya kumsahau Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Seif Sharif Hamad.
Hawa wote wameorodhesha kwa njia moja au nyengine kwamba UTAWALA WA TANGANYIKA KWA KIVULI CHA MUUNGANO umefikia ukingoni.
Darubini yetu inaangalia . Jee, Zanzibar imejifunza nini kutokana na utawala wa mabavu, ukoloni wa kitanganyika kwa miaka 49 iliyopita?
Jee, Tanganyika iko tayari kuliachilia koloni lake la Zanzibar kwa miaka 49?
Jee, Watanganyika wameisaidia nini Zanzibar?
Jee, Watanganyika wameijenga Zanzibar au kutia umasikini kwa miaka 49?
Darubini yetu inawaachilia wana Mzalendo kutoa maoni yao.
Kwaheri mkoloni Tanganyika kwa kutumia ujanja wa Muungano wa kitapeli kuitawala Zanzibar, Utawala wa kimabavu na wizi umefikia ulingoni.

Chanzo: Mzalendo

1 comment :

  1. Muungano wenye kupata ridhaa ya wananchi wa nchi zinazoungana ni muungano wa uhakika na ule wa mabavu basi huwa ni wa muda tu.Kusema kweli Zanzibar imepoteza hadhi yake kiuchumi,utamaduni,elimu na ustawi wa jamii kwa ujumla.Ikipata fursa ya kujumuika na wale wenye kutaka kuiona Zanzibar inapiga hatua kimaendeleo,basi haitachukua miaka 49 lakini itachukua miezi 49 kuonekana mchomozo wa NURU YA TAA KATIKA KIZA KILIOPO HIVI SASA.

    ReplyDelete