Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, January 10, 2013

NASSOR MAZRUI: Waziri Mazrui na Karafuu Zetu

 A Liberator who has now become a Dictator!

Written by   //  10/01/2013

Moja ya ‘milestone’ waliyokuwa wanaringia sana GNU ni kupandisha bei ya karafuu. Na wananchi wa Zanzibar na hasa Pemba ambalo zao la karafuu linazaliwa kwa wingi, walikuwa wakipiga vigelele kwa furaha.
Kwa kiasi kikubwa, bei mpya iliwakomboa wananchi wa Zanzibar; na hali ya umasikini kidogo ilipungua, makali ya maisha yalipungua; ingawa bei za bidhaa muhumi ilizid kupanda.
Hali imebadilika, na bei ya karafuu imeshuka sana katika soko la duni [sina takwimu sahihi, anayejua atupatie data hizo muhumi, bei ya karafuu katika global market].
Kwa vile bei imeshuka, wakulima na wachuuzi wa zao hilo, wamekuwa wagumu kuiuzia serikali (ZSTC), na wametafuta mbadala wake ‘wanaujua wenyewe’.
Sasa imekuba balaa, Waziri Wa Biashara, Mstahik Nassor Mazrui anasema ‘lazima wakulima wauze karafuu zao ZSTC, na wasiotaka kutii amri hiyo ama wakamatwe, au mali itaifishwe, na kuamrisha vikosi vya vya SMZ viwe ‘vigilant’ wawasakame, na wawakamate na kuwachukulia hatua za kisheria’. Very authoritarian language — na lugha za kibabe, jeuri za kiutawala.
Kutokana na ‘fatwa; hiyo ya sahib yangu Mazrui, matukio mengi mabaya yameaanza kujitokeza hasa Pemba, kukamatwa watu bure bure, hasa maeneo ya mwambao wa bahari, kutupiana risasi baina ya KMKM na wenye vyombo vya baharini kama vile ngalawa, mashua, jahazi n.k.
Inasikitisha kusikia na kuona amri kama hizi anazitoa mtu kama Mazrui, mtu /mfanyabiashara, mwenye asili yeye, babu zake, wazee wake wote wamekulia na kutokana na bishara ya karafuu, anaijua A-Z kama dr.Shein anavyoijua hosp ya Mnazi Mmoja — dam dam.
Mazrui na Mohammed Aboud (super boy) wanaijua biashara ya karafuu kama jina zao — mmoja wa Mkanjuni akitokea kwenye asili Mitamani, mwengine wa Wara (wawi).
* Mazrui anaijua vizuri sana karafuu ni nini – enzi zile wakulima wakipewa majamvi, kapu na magunia bure – leo zinaanikwa chini, magunia ni mapolo ya mapembe (recycable…..?). Leo yapo wapi hayo, wakulima wanaumia na mtutu wa bunduki unawasubiri.
Kama mantik ya Mazrui ni hiyo, kuwa lazima tutumie MTUTU wa BUNDUKI kwa kila national program, kwa kila kitu katika maisha yetu — kuanzia kuandika sensa, kuandika kura na kupiga kura, kuandikisha National ID, kutoa maoni ya katiba — yote haya lazima UTUMIKE MTUTU WA BUNDUKI  ndio tunakwenda. Kweli tutapiga hatua kiasi gani.
Mimi natoa challenge kwa Mazrui kama kweli bingwa, kwa nini haingilii kupandishwa kwa bei ya bidhaa muhimu hapa Zanzibar — mchele, sukari, unga n.k hizi bidhaa zinapanda kila siku kama vile unavyoona shares zinavyoshuka na kupanda pale New York Stock Exchange. Hakuna jutification ya kupanda bidhaa kiasi hicho — kisingizio ‘dola imepanda, dola imeshuka’.
Pili, kama yeye hodari sana — mpaka leo Zanzibar tunakula low quality mchele wa mapembe, na yeye alisema ‘mapembe yatakuwa basiiiiiii’.
Juzi tu bandarini umekamatwa mchele tani 45 wote mbovu, unga tani zaidi ya 50 wote mbovu. Haya yamemshinda, lakini kuwahilikisha jamaa zake, wakulima wa karafuu anaweza kuamrisha vikosi vya SMZ iwatandike bakora sawa sawa.
Jamani kuongoza sio kutumia mtutu wa bunduki, ni busara zaidi – inatakiwa ujue source ya tatizo, na kulitatua katika misingi ya busara ya umahiri zaidi. Sisi kila kitu MTUTU WA BUNDUKI, mara moja hata chanjo za watoto vikosi vya SMZ vilikuwa vinapita kila nyumba kulazimisha watoto wachanjwe, dawa ya kuulia mbu, pia ilikuwa vikosi vya SMZ vinalazimisha lazima upigiwe dawa. AKILI ZETU ZIMEFUNGIKA HAPO, KUWA MTUTU WA BUNDUKI NDIO SULUHISHO, basi hata kupigiwa dawa ya mbu, au chanjo.
Mimi naomba sana SMZ ibadilishe approach yake kwa wananchi wake, tumewafanya wananchi/raia wamekuwa sugu sana kiasi ambacho kimezaliwa kitu ‘lawlessness’ katika jamii zetu. Imezaa usugu wa watawaliwa (wananchi) na usugu wa watawala — kuwa wao ndio wao tu, ambayo huzaa jeuri na kiburi cha utawala.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment