Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 9, 2013

ZANZIBAR: DR SHEIN ASISITIZA UTUNZWAJI WA BARABARA

Written by   //  09/01/2013

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameuagiza uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kuziwekea  Mipaka maalum barabara zinazojengwa Zanzibar ili Wananchi waepuke  kujenga pembezoni mwa barabara hizo.
Hayo ameyasema jana huko Bumbwini-Mfenisini wakati wa ufunguzi wa barabara  hiyo ikiwani ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya  Mapinduzi ya Zanzibar.
Dkt. Shein amesema kwa kufanya hivyo kutaisaidia Serikali kuepukana kuwalipa fidia Wananchi ambao wanatabia za kujenga katika maeneo ya barabara kwa kutarajia malipo pale nyumba zao zitakapobomolewa kufanya utanuzi wa  barabara hizo.
“Mnawachia watu wanajenga pembezoni mwa bara bara wakati mnawaona, mtu anaaza  msingi, anainua tofali, anaezeka ,na anapiga palasta na nyinyi  mnashuhudia,lazima iwekwe mipaka ya kuonesha eneo hili halipaswi  kujengwa na atakae jenga avunjiwe .”alifahamisha Dkt.Sheini.
Alisisitiza kuwa babara ina mipaka yake maalum na kwamba mtu atakayebainika kujenga nyumba kwenye mipaka hiyo lazima ivunjwe kwani mtu huyo atakuwa  anakwenda kinyume na taratibu za bara bara.
Dkt. Shein alitoa mfano wa barabara zilizojengwa nyumba pembezoni ambazo  zinatarajiwa kutanuliwa siku za karibuni kuwa ni bara bara ya  Magomeni-Kwerekwe na barabara ya Bububu kuelekea Mkoa wa Kaskazini  Unguja.
Alisema bara bara hizo ziliwekewa maeneo yake kwa ajili ya utanuzi siku za  usoni lakini hakukuwa na mkakati wowote wa kulinda mipaka ya barabara  hizo jambo ambalo liliwapelekea wananchi kupuuza sheria kwa kujenga  nyumba.
Aidha Dkt. Shein aliwataka watendaji wa Wizara hiyo kuzitunza vyema Bara bara hizo alizozizindua pamoja na Madaraja manne ikiwa ni pamoja na kupanda  miti pembezoni na kuepusha kuchomwa moto kwa kutumia matairi ili  zisipoteze kiwango chake.
Nae Mwakilishi mkazi kutoka AFDB Bank Bi Toniya Kandiyero alisema kuwa Bank yao ipo mstari wa mbele kusaidia maendeleo ya Zanzibar katika miradi  mbalimbali ambapo kwa upande wa Barabara imesaidia takribani Kilomita 83 katika maeneo ya Unguja na Pemba.
Bi Toniya alisema kwa sasa benki yake imejipanga kusaidia maeneo mengine  mapya kama vile mazingira ya bahari na raslimali zake pamoja na shughuli zinazo fanywa baharini.
Bara bara ya Bumbwini-Mfenisini imejengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya  kizalendo ya MECCO ambayo inaurefu urefu wa kilomita 13.2 ikiwa ni msada wa fedha kutoka bank ya Afrika  AFDB.

Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment