Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 9, 2013

ZANZIBAR: Dr Shein na Shutma za Kuishushua ZBC

Written by   //  09/01/2013

M/Mungu amemuumba binaadamu kwa umbo lilobora, kisha kamfundisha njia mbili imma ashukuru au akufuru.
 Hapo jana sikuamini masikio na macho yangu pale niliposikia na kuona Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein katika ufunguzi wa mradi wa Digital, anasimama hadharani na kukiksema chombo chakee adhimu cha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
 Dr Shein alitowa shutma nzito dhidi ya ZBC kwa kusema “…(ZBC) sasa imekua ndio ya mwisho kutokana na utendaji wake”. Hakuishia hapo Dr Shein aliendelea kusema “uendeshaji mbovu wa vipindi visivyo na mahitaji kwa jamii
 Nimepokea lawama hizi kwa mshangao mkubwa, kwani nilikuwa miongoni mwa Wazanzibar wengi waliopinga tokea uundwaji wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar mpaka kufikia uteuzi wa wakurugenzi wake. Hoja za kupinga kwangu zilikuwa sababu tatu kuu:
i)                    Huwezi kuwa na shirika moja lenye wakurugenzi watatu kwa wakati mmoja. Huu ni upotevu wa resources na kuviza utendaji kazi.
ii)                   Wakuregenzi waliopewa shirika hili ndio walewale waliokabidhiwa hapo kabla na kulifikisha hapo lilipo. Mfano mmoja nilioutowa ni ule wa jengo la Sauti ya Zanzibar pamoja na kuwekewa vifaa vipya, baada ya miaka 15 vyote vimeshatupwa.
iii)                 Tunaingia kwenye mfumo wa Digital, hii fani haitaki Mkurugenzi mwanasiasa, mwanasheria, mwandishi, au vyenginevyo. Anayehitajika ni Mkurugenzi Technical Compitant, innovative and creative.
 Nani hamjuwi Mkurugenzi Hassan Abdalla Mitawi utendaji, ufanisi, majungu na mascandal yake. Ikumbukwe vifaa vile vya TV kule Pemba vilivyozama baharini hakuna taarifa yoyote iliyopatikana.
 Vipi kuhusiana Mkurugenzi Sufiani Khamis Juma, licha ya umri wake na hali yake kudhoofika siku hadi siku, lakini utendaji na ufanisi wake unadhani ungeliweza vipi kuisaidia Television Zanzibar kuhuika. Ikumbukwe hivi karibuni waliwashusha vyeo wahariri wawili kwa kosa la kuonyesha muda mrefu zaidi taarifa ya Makamo wa Kwanza wa Rais kuliko Rais mwenye.
 Jee kwa Mkurugenzi Rafii Haji Makame elimu, utendaji, ufanisi wake ungeweza vipi kuisaidia Sauti ya Zanzibar kuchechemea na angalau kuyarudisha majengo kwenye hadi yake.
 Siku zile wakati natowa mapungufu haya wako waliodhani kwamba napigania nafasi ile, laaa, nilikuwa naelezea kile ninachokiamini na kilichokuwa ndicho, kwamba Wakurugenzi wote hawa hawana uwezo wa kulihuisha Shirika la Utangazaji la Zanzibar.
 Kwako Dr Shein amini usiamini, binafsi nimmoja mwenye imani kwamba unayodhamira ya kweli kuibadilisha Zanzibar, hivyo lichukulie suala hili kwa SERIOUS hasa katika uteuzi wa Mkurugenzi wa ZBC. Hivi karibuni mswada wa sheria ya Kuanzisha Shirika la Utangazaji utawasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi tunaomba kuwe na mfumo mpya wa kumpata Mkurugenzi wa ZBC. Naye apatikane kwa njia ya maombi. Nafasi itangazwe wenye moyo na sifa waombe na mwisho yule atakaeshinda akabidhiwe ofisi kwa mkataba usiozidi miaka 3. Kamati ya Baraza la Wawakilishi katika masuala ya habari ndio isimamie upatikanaji wa Mkurugenzi huyu.
 Dr Shein vyombo vya habari ni kioo na nyenzo  ya kuitangaza na kuiuza nchi mbele ya nchi nyengine. Tutakapokuwa na Mkurugenzi mwenye sifa bora sinashaka lengo lako litafikiwa.
 Dr Shein vyombo vya habari ndio mdomo wa serikali kwa wananchi wake pale inapotaka kuelimisha jamii. Hivi leo iweje taarifa zako hata wananchi wako hawazipati kupitia vyombo hivi ambavyo fedha za utendaji wake zinatoka chini ya sign yako.
 Dr Shein mengi mazuri serikali yako iliyofanya hadi leo hii wananchi wako hawayatambui kwa kukosekana ubora ZBC. Bila ya shaka hii itakuwa nafasi muhimu nchi yetu kuona vyombo vyetu vya habari vinakuwa tayari kufikia lile lengo lililokusudiwa.
 Tuko tayari kukusaidia ikiwa ni ushauri, utendaji au vyenginevyo. Tafadhali usiche kutuona.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment