
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Ltd) imetujulisha rasmi kuwa inashirikiana na kampuni moja ya kupeleka pesa nyumbani yenye bei nafuu kuliko Western Union au MoneyGram kupitia internet (yaani online). Kwahivyo, Mwana-Diaspora unaweza hivi sasa kupeleka pesa Zanzibar na Tanzania nzima kutoka nyumbani kwako, bila ya kuenda benki au kuenda exchange house yoyote ile. PBZ imeanza tokea tarehe 31 January, 2013, kutoa huduma hii, kwani inafahmau kuwa huku nje tunakoishi muda hatuna wa kuenda huku na kule.
Ukitaka kupeleka pesa nyumbani, process yenyewe ni fupi sana na ni kama ifuatavyo:
[1] Unakuenda kwenye website hii hapa: www.worldremit.com
na hapo unajiandikisha kwanza.
[2] Ukitaka kupeleka pesa Zanzibar au Bara zipo 3 easy steps ambazo hata mtu mwengine hanahaja ya kukuelekeza – it’s so simple and straight forward kutoka kwenye website!
Zaidi ni kuwa, upo uhuru wa kuweza ku-fix amount unayotaka kupeleka, either in Canadian Dollars or in TShs na baadae system itakupa gharama zako zote in Canadian Dollars (kama upo Canada) – yaani unaweza kujaza, say, 100 Dollars unataka kupeleka, au unataka mtu wako apokee TSHS 50,000/-. Pia, unaweza kupeleka kiasi chochote kile. Minimum ni $15 na minimum fee nadhani ni $1.99 kama hivi. Kwahivyo, sio lazima uwe na pesa nyingi ndio utake kupeleka pesa nyumbani.
[3] Ukesha ku-click submit button, baada ya dakika kidogo utaletewa email msg isemayo kuwa your transaction was being processed. Kama umejaza sawasawa kila kitu ulichoulizwa, basi baada ya dakika 2-3 nyengine utapata email msg yapili inayokueleza kuwa your transaction was successful na anangojewa mtu wako Zanzibar akapokee pesa kutoka PBZ Ltd - branch ya Malindi kwa Zanzibar, Chake Chake kwa Pemba na Kariakoo kwa DSM.
[4] Yule unaempelekea pesa kule ZNZ yeye atapata SMS msg kwenye simu yake na email msg pia akielezwa kuwa umempelekea pesa na anatakiwa aende PBZ kuzichukua. Kwa upande wao PBZ hawatakiwi wafanye lolote isipokuwa kulipa tu, kwani kila kitu kinakuenda automatic. Lakini, juu ya hivyo naona PBZ wanasaidia sana, kwani wanampigia simu mtu uliempelekea na kumueleza kuwa akachukuwe pesa zake. Mtu uliyempelekea pesa akizichukua tu kutoka PBZ wewe huku ughaibuni utaletewa email msg pamoja na SMS msg kukujulisha kuwa jamaa yako uliempelekea pesa Tanzania keshachukuwa pesa kutoka PBZ Ltd. Kwahivyo, hunahaja ya kupiga simu ZNZ ukagharimika zaidi!
Ni process rahisi sana na haichukuwi hata dakika 2 kuimaliza.
Pia, ifahamike kuwa tunaweza kufungua foreign currency accounts pale PBZ wakati tupo huku nje!
OMBI:
Tunachoomba ni kuwa kila mtu amjulishe mwengine juu ya hio address ya website ya World Remit. Pia, tunataka watu waitembelee hii website na wajaribu kutaka kutuma pesa Zanzibar hata kama mtu hataki kupeleka pesa hivi sasa. Just jiandikishe tu kwenye website ili ukipata emergency ya kupeleka pesa utakuwa hunahaja tena ya kupoteza muda kwa registration.
Sote tunajua kuwa hatuna uwezo wa kuisaidia nchi yetu ya Zanzibar kama vile ambavyo tungelipendelea, lakini kila mtu anapeleka pesa nyumbani kwa ndugu, wazee na jamaa zetu. Kama tutazipitisha hizo pesa tunazozipeleka nyumbani japokuwa ni kidogo kwa njia ya PBZ Ltd huo bila ya shaka utakuwa msaada mkubwa sana kwa nchi yetu, kwani utaiwezesha nchi yetu kupata foreign currency.
Jirani yetu nchi ya Kenya leo inapokea kama Dollar billion 2 kutoka Wakenya wanaoishi nje kwa kila mwaka. Japokuwa wenzetu wapo wengi nje, lakini pia hii inaonesha kuwa wanamoyo wa kuisaidia nchi yao. In fact, Africa yote inapokea kama 60 billion Dollars kila mwaka, lakini kwa Zanzibar ni sehemu ndogo sana inayofika serikalini kwa faida ya nchi yetu kutokana na hicho kidogo kinachopelekwa. Kwahivyo, njia pekee ya kuiwezesha nchi yetu ni kutuma pesa nyumbani kupitia Benki ya Watu wa Zanzibar!
Shime shime wazalendo
tuisaidie nchi yetu!
Chanzo: Zanzibar-Canadian Diaspora Association (Toronto, Canada)
No comments :
Post a Comment