Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 6, 2013

Dk. Shein ahimiza mafunzo ya ufundi

NA MWINYI SADALLAH

6th March 2013

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
Rais wa  Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, amesema mafunzo ya ufundi yana umuhimu mkubwa katika kuongeza ajira kwa vijana na kufanikisha mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi wake.

Dk. Shein alitoa tamko hilo jana baada ya kuzindua kituo cha kazi za ufundi huko Chumbuni katika ziara yake ya kwanza ya mikoa mitano ya Visiwani Zanzibar.

Alisema mafunzo ya ufundi  yana umuhimu mkubwa katika maisha ya mwanadamu ndiyo maana serikali yake ikaamua kuweka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ambayo unasimamia kutoa mafunzo ya ufundi.Kutokana na hilo, Dk. Shein alipongeza juhudi za mradi wa TASAF kwa kuwaunga mkono wananchi kwa kuwaonesha njia katika kujiletea maendeleo endelevu huku akitumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa viongozi wa jimbo akiwamo Mbunge kwa kuwasaidia wananchi katika kuendeleza kituo hicho.

Dk. Shein pia alitoa pongezi kwa wajasiriamali hao kwa kuwa na azma ya kuanzisha mafunzo ya uwashi na usaramala na kuisisitiza kamati ya kituo hicho kuanza masomo hayo haraka ili yawasaidie  wananchi wakiwamo vijana ili kupata elimu na hatimaye kuajiriwa ama kujiajiri wenyewe.

Aidha, Dk. Shein aliwataka wale wote watakaopata mafunzo katika kituo hicho kufuata maadili ya kazi zao ili wajijengee mustakabali mwema katika jamii hatua ambayo itawasaidia kupunguza makali ya maisha.

Katika hotuba yake, Dk. Shein aliahidi kuwaunga mkono wajasiriamali hao kwa kuahidi kusaidia kompyuta mbili pamoja na vyarahani vitatu huku akikubali kuwa mlezi wa Kituo hicho.   Wajasiriamali hao walipongeza juhudi za serikali kupitia mradi wa TASAF kwa kuwaunga mkono katika shughuli zao hizo pamoja na kuwapongeza viongozi wao wa Jimbo kwa kuwaunga mkono.

Katika ziara yake, Rais Dk. Shein alikagua miradi ya elimu ikiwamo ujenzi wa shule ya sekondari ya Wilaya iliyopo Mpendae, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment