NA EDITOR
15th March 2013

B-pepe

Chapa

Maoni
.jpg)
Majambazi hao pia walimjeruhi kondakta wa Hiace hiyo, George Athoni, kwa kumpiga risasi katika miguu yote kisha kumpora Shilingi 250,000.
Tukio hilo lilitokea jjuzi asubuhi katika pori lililoko katika kijiji cha Kishanga wakati gari hilo likisafiri likiwa na abiria 16 kuelekea mjini Kigoma.
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma lilithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa majambazi hao walifyatua risasi na kumlazimisha dereva wa Hiace kusimama hivyo kutoa nafasi kwao kuingia ndani ya gari na kuanza kuwavua nguo abiria kisha kupora mali zao.
Tukio hilo ni jipya kutokea hivi karibuni kutokana na vyombo vya usalama hususani Jeshi la Polisi kufanya doria za mara kwa mara na wakati mwingine kuyasindikiza magari ya abiria kupita katika maeneo ya mapori ambayo hutumiwa na majambazi kuteka magari na kuwapora abiria.
Huko nyuma, kulikuwapo na matukio mengi ya majambazi kuteka mabasi na kuwapora abiria mali katika maeneo yanayozungukwa na misitu na mapori.
Baadhi ya mikoa ambayo matukio hayo yalikuwa yamekithiri ni Kagera na Kigoma kwa kutaka michache. Mikoa hiyo iliathiriwa sana na matukio hayo kutokana kuhifadhi idadi kubwa ya wakimbizi ambao baadhi yao walijiingiza katika uhalifu.
Utaratibu wa Jeshi la Polisi wa kufanya doria za mara kwa mara pamoja na kuyasindikiza magari ya abiria ulipunguza matukio hayo kwa kiwango kikubwa.
Tukio la juzi la kutekwa kwa Toyota Hiace na kuwadhalilisha abiria kwa kuwavua nguo na kuwapora ni salamu kutoka kwa majambazi kwamba wamerejea kwa nguvu mpya, hivyo ni changamoto kwa Jeshi kwamba linapaswa kujipanga kukabiliana na hali hiyo.
Kinachodhihirisha hilo ni kitendo cha majambazi hao kutenda uhalifu huo saa moja asubuhi bila wasiwasi wala woga kwamba wanaweza kukamatwa.
Jeshi la Polisi halina budi kufahamu kwamba wanaofanya vitendo vya kuteka magari ni watu wenye mbinu na ni hatari kwa kuwa wanamiliki silaha za moto. Ndiyo maana katika tukio la juzi majambazi hao walikuwa na bunduki waliyoitumia kumpiga risasi kondakta wa Hiace.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema kuwa limeanza msako wa kuwasaka majambazi hayo ili wafikishwe katika vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake.
Pamoja na Jeshi la Polisi kufanya msako, kuna haja ya kutafutwa mbinu mpya na endelevu katika kukabiliana na wimbi la uhalifu wa kuteka mabasi, vitemdo ambavyo vinahatarisha usalama wa raia na mali zao.
Miongoni mwa hatua ambazo zinawezakusaidia kudhibiti vitendo hivyo ni serikali kujenga vituo vya polisi karibu na maeneo ambayo matukio hayo yamekuwa yanatokea mara kwa mara.
Vile vile, kuna haja kwa Jeshi la Polisi kufanya operesheni za mara kwa mara za kuwasaka majambazi katika maeneo hayo sambamba na dorua zenye uhakika.
Huko nyuma aliyekuwa Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Venance Tossi, alikuwa akiongoza operesheni za mara kwa mara katika maeneo yaliyokuwa yanatumika kufanya vitendo vya ujambazi.
Operesheni za Tossi zilisaidia sana kupunguza matukio ya uhalifu kwa kuwa majambazi wengi walitiwa mbaroni na wengine waliuawa na hivyo wananchi kuishi katika hali ya usalama.
Kwa kuwa Jeshi la polisi ni taasisi, linapaswa kutekeleza majumuku yake ya kudhibiti ujambazi kwa kasi ile ile aliyoitumia Tossi.
Hatupaswi kusubiri athari kubwa zaidi zitokee kutokana na kukithiri kwa ujambazi bali hatua za haraka zichukuliwe ikiwamo kubuni mbinu mpya za kudhibiti majambazi wanaoteka mabasi.
Tunaamini kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuwasjirikisha wananchi katika kukabiliana na tishio hilo kupitia mpango wa ulinzi shirikishi.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment