AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, April 23, 2013

Benki ya Dunia kusambaza umeme Biharamulo Vijijini

Na Salum Maige, Mwananchi  (email the author


Posted  Jumanne,Aprili23  2013  saa 10:26 AM
KWA UFUPI
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufunga Umeme Vijijini (RESCO), Mzumbe Mussa, alipokuwa akizungumzia shughuli zinazotarajiwa kutekelezwa na kampuni yake kwenye zahanati na sekondari katika vijiji hivyo.
Biharamulo. Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) zinatarajia kusambaza umeme wa mionzi ya jua katika zahanati sita na shule sita za sekondari katika vijijini vya Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufunga Umeme Vijijini (RESCO), Mzumbe Mussa, alipokuwa akizungumzia shughuli zinazotarajiwa kutekelezwa na kampuni yake kwenye zahanati na sekondari katika vijiji hivyo.
Mussa alisema hatua hiyo inalenga katika kuwaboreshea mazingira ya kuishi kwa watumishi wa zahanati hizo.
“Lakini pia tunaamini hatua hii itasaidia sana kuwawezesha wanafunzi kujisomea kikamilifu nyakati za usiku maana watakuwa na umeme wa uhakika,” alisema.
Mussa alisema lengo la msaada huo ni kuisaidia serikali kuboresha huduma kwa wananchi wa vijijini wanaokabiliwa na changamoto za ukosefu wa nishati ya umeme.
Alibainisha kuwa Benki ya Dunia imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo. Zahanati zitakazonufaika na msaada huo ni Kalenge, Nyakanazi, Ngalalambe, Katahoka, Kasozibakaya na Mbindi.
Kwa upande wa wa shule ni za Runazi na Nyantakara

No comments :

Post a Comment