AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, April 16, 2013

Bila ya mashirikiano ya serikali na wana mazingira malengo hayatafikiwa

Picha ya pamoja ya wanachama  wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliowachagua viongozi mbalimbali wa Jumuiya hiyo
Picha ya pamoja ya wanachama wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliowachagua viongozi mbalimbali wa Jumuiya hiyo
Imelezwa kuwa iwapo patakua na mashirikiano katika Jumuiya ya  Uvuvi na  Mazingira Endelevu Zanzibar (ZFSE) iliyopo  Mtoni  Kidatu hakuna sababu ya umoja huo kutoyafikia malengo waliyojipangia…
 Hayo yamelezwa na Mwenyekiti wa ZFSE  Sheha Chumu Mngana wakati alipokuwa akizungumza  na wanjumuiya hiyo baada ya kuchaguliwa  rasmi kuongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu katika uchaguzi uliofanyika skuli ya  sekondari  ya JKU Mtoni nje kidogo ya Mji wa  Zanzibar.
Amesema ni vyema  kwa Jumuiya  hiyo kutekeleza majumu yao   waliojipangia pamoja na kubuni miradi mbali mbali ili kuleta maendeleo katika Jumuiya yao.
‘’Bila mashirikiano, hatutofikia popote, kuwa makini au kujielewa na kutekeleza majukumu na kila mwanachama anawajibu wa kupatiwa haki’’ Alisema Sheha Chumu Mngana.
Katika uchaguzi huo  wamechaguliwa wajumbe wanne wa Kamati Kuu  ikiwa ni njia mojawapo ya kuipa nguvu jumuiya hiyo  ambao ni  Zena Husein Suwedi, Haji Khamis Hassan,  Mansab Ramadhan Mansab na Mashavu Mzee Moh’d.
Aidha Mwenyekiti  Sheha Chumu  amesema   Jumuiya yao  yenye wanachama 20 wakiwemo wanaume 10 na wanawake 10  inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika  ikiwemo ofisi ya kudumu  pamoja na vitendea kazi  jambo ambalo linapelekea kukwamisha  ufanisi wa Jumuiya yao.
Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar ilianzishwa mwaka jana na  imepatiwa  usajili rasmi tarehe 12 /4/ 2013  na Mrajisi  Mkuu  wa Serikali  Nd. Abdallah Wazir.

Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment