Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, Omar Mussa Makame (35) aliyevaa shati la rangi ya waridi akiwa Mahkamni kwa mara ya kwanza.
Zanzibar
Mahakama Kuu ya Zanzibar itatoa uamuzi iwapo impe dhamana Omar Mussa Makame (35) anayetuhumiwa kumuua Padre Evaristus Mushi Aprili 29 mwaka huu…
Mahakama Kuu ya Zanzibar itatoa uamuzi iwapo impe dhamana Omar Mussa Makame (35) anayetuhumiwa kumuua Padre Evaristus Mushi Aprili 29 mwaka huu…
Jaji Mkusa Isaac Sepetu alipanga tarehe hiyo jana katika Mahakama Kuu ya Vuga mjini hapa baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili – upande wa mashitaka na upande wa utetezi.
Upande wa mshitaka ukiongozwa na Abdallah Issa Mgongo uliiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine kwa madai kwamba ushahidi bado haujakamilika.
Wakili wa utetezi, Abdallah Juma alipinga hoja hiyo akidai kwamba Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alitangaza hadharani kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika.

Alidai kuwa anashangaa sasa kumsikia mwendesha mashtaka akidai haujakamilika huku akihoji ni ushahidi gani anaoutaka wakati Polisi wanaohusika wanaeleza kwamba wamekamilisha.
Wakili Juma aliiomba Mahakama imwachie kwa dhamana mshitakiwa ili ushahidi utakapokamilika aletwe tena mahakamni kuliko kunyimwa haki kwa kusota rumande.
Mgongo alidai kuwa suala hilo si kumuonea mshitakiwa kwa vile ushahidi haujakamili bali ni kutenda haki na utakapokamilika utaletwa mahakamani mara moja.
Padre Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya mji wa Zanzibar na mtuhumiwa alitiwa mbaroni na Polisi tangu Machi 17 mwaka huu.
Chanzo: ZanzibariYetu
No comments :
Post a Comment