zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 1, 2013

Sitta atengewa Bilion 20.5

Na Salome Kitomary

1st April 2013
                                              Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.
 
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imepitisha makadirio ya bajeti ya zaidi ya Sh bilion 20.5 ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2013/14.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Lowassa, alitoa kauli ya kupitishwa kwa bajeti hiyo mwishoni mwa wiki, wakati akihairisha kikao cha kamati hiyo, kutokana na msiba wa mjumbe wa kamati hiyo, Mbunge wa Chambani (CUF), Salim Hemed Khamis, aliyefariki Alhamisi.

“Pamoja na msiba uliotupata, lakini natamka bajeti ya wizara hii imepitishwa kwa ajili ya vitabu vya Hazina, lakini tutaipitia kipengele kwa kipengele tutakapokutana mkoani Dodoma,” alisema Lowassa.

Awali, wajumbe wa kamati hiyo, walitaka kuwajua ni kwanini vikao vya bunge hilo havifanyiki nchini na kusikia vikiendelea kwenye nchi za wengine na kuwataka wabunge hao kuhakikisha vikao hivyo vinafanyika nchini.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment