AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 18, 2013

Unyanyasaji katika Airport na bandarini Z’bar wazidi’

Written by   //  18/04/2013 
Structure ya jengo la uwanja mpya wa ndege Zanzibar
Structure ya jengo la uwanja mpya wa ndege Zanzibar
 Kutangazwa kuwa Zanzibar ni kituo kikuu cha uingizaji wa Madawa yakulevya , wahanga wengi wamekuwa ni abiria wa kawaida wasio husika kabisa na mambo hayo.
Hii askari wa Kastamu wameichukulia kama mwanya wa kutumia vyeo vyao ili kutisha kwa kupata chochote kutoka kwa abiria waingiao na watokao, kusumbuliwa na kunyanyaswa imekuwa ndio biashara ya kubinya abiria ili wapate chochote kutoka kwa kwenye mabegi yao au kwenye vipochi.
Kuna kesi nyingi tu za unyayasaji hivi sasa zidi ya raia wakawaida kwa kutumia kigezo cha kusasambuliwa vitu kwa kusema wanatafuta dawa za kulevya sio mbaya lakini , upekuzi wao umefurutu mipaka na lengo sio hilo ni kutengeneza pesa kwa njia ya kutisha .
Unapofika Bandarini au Air Port mfano unapidisha mizigo yako katika machine ya scan , hio haitoshi baada ya hapo vitu vyako vina sasamburiwa sasa kwa mikono hazarani bila kujali kuwa vitu vyengine kama nguo za ndani za wanawake na vitu vyengine .
Hapo kinachofanywa ni kuja askari wa kastamu kuanzia 3-4 wanakusimamia na kukuzonga kwa maneno ili wale wenye kupekura wapate kuiba na ukifika nyumbani utakuta kuna vitu vimebungua too late tena.
Tukiachana na hilo ukijifanya msemaji wanatumia vitisho vyakusema nenda migombani kamueleze Maalim Seif Shariff yeye ndie alio tutuma na ni kitengo chake hichi cha Madawa yakulevya sio sisi ,sisi tunafanyakazi yetu tu tulio pewa.
Lakini chakushangaza nikuwa na kutia hudhuni kuhisi kuwa haya ni manyanyaso zidi ya usumbufu, jee kuna faida gani ya hizo machine za scan? au hata kama beg lina nguo tu za kikke nilazima zijulukane ?
Hii mimi nasema ni unyanyasaji na kusasambura kila kitu kwa mila zetu vikiwemo vitu vya kikke ni aibu na kutafutwe mbinu nyingine na machine zaidi kuliko wizi huu wakunyanyasa abiria walochoka kisafari na kuja kuwatesa na kuwasumbua kwa kisingizio cha madawa yakulevya.
Askari hao hao wa kastam na Air Port ndio wenye wenye kula na waingizaji na watowaji wa madawa yakulevya na wao wanawajua fika sio kuwasumbua abiria wakawaida na dada zetu kuwakashifu pale.
Wauzaji wakubwa wa unga mabegi yao yenye unga hayapekuriwi na huingizwa kabla ya hata wao kufika , na waingizaji ni hao hao askatri musitusumbue, kuna wazungu wa kitaliana na wafanya biashara wakubwa huingiza unga na kutowa hapo bila kusachiwa au kusimamishwa wanakuwa VIP yote hayo yanajulikana.
Hii inayofanywa hivi sasa nikumpaka Matope Maalim Seif kwa kuhujumu Bandari na Air Port kwa kuwa vijana wengi hivi saa wa kiZanzibar wanateremkia Zanzibar hususani nduguzetu wanao ishi Uk.
Hivi kweli ina ingia akilini Mtu anatoka Uengereza aingie na Dawa zakulevywa hapo? wakati kapita katika nchi kama 3 transit na zote hizo zina security ya hali ya juu, kweli leo autowe Unga Europ aje auze Zanzibar ina make Sense kweli hii?.
Hii ni kampeni tu yakuaa Air port ya Zanzibar kwa vile kila abiria nilazima alipe Dollar 100 kila kichwa sasa imeonekana ili watu wateremkie Bara tufanye hivi na chanzo kimepatikana na mwiba umechoma pazuri huu usumbufu wa madawa yakulevya.
Kwa vile kitengo hichi ni katika wizara ya Maalim Seif basi swala hili linachukuliwa kisiasa zaidi ili kumpaka matope na kazi hii inafanywa na jibu husema askari wa Air port na Kastam kuwa nenda Migombani kamwambie alotutuma makamo wa Kwanza wa Rais Maali Seif.
Kama Smz hawakujipanga vizuri na bugza hii itaendelea basi hakuna haja yakupanua kiwanja kipya maana abiria wote watashukia Bara na Zanzibar itakuwa wapunga nzi tu hakuna mwenye kutoka safari halafu akaja kubukuziwa na kusumbuliwa huku kachoka.
Tunaomba kufanyiwe marekebisho mara moja kama tunataka maendeleo ya nchi yetu.

Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment