AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, April 16, 2013

VITA DRC: M23 wanatapatapa, asema Mwambene


Na Amini Yasini, Mwananchi. 

Posted  Jumanne,Aprili16  2013.
KWA UFUPI
Serikali imesema haitasita kupeleka askari wake Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kwa ajili ya kukabiliana na waasi wa kikundi cha M23 .
Serikali imesema haitasita kupeleka askari wake Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kwa ajili ya kukabiliana na waasi wa kikundi cha M23 .
Imesema hatua ya kikundi hicho kuionya Tanzania kutopeleka askari wake huko ni ya kutapatapa.
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene, aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana asubuhi kuwa Tanzania haitishiki na kauli ya waasi ya kushambulia askari wa Tanzania.
Alisema vitisho hivyo ni dalili za wazi kwamba waasi wanalijua Jeshi la Tanzania ndio maana wanatapatapa
Mwambene alisema Tanzania imeamua na itafanya kazi hiyo kwa mwavuli wa Umoja wa Mataifa, lengo likiwa ni kuleta usalama katika ebneo la Mashariki ya Congo.
Msemaji huyo alisema wanajeshi wa Tanzania wataungana na wanajeshi wa Afrika Kusini na Malawi katika operesheni hiyo muhimu.
Kauli hiyo inafuatia madai kuwa uongozi wa kikundi hicho, umwandikia Rais Jakaya Kikwete, kumtaka afikirie upya wazo la kuwapaleka askari wa Tanzania katika Brigedi ya Umoja wa Mataifa ya kuwalinda raia katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.  
 

No comments :

Post a Comment