AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 17, 2013

Mbunge ahoji matumizi ya fedha za wahisani




JIBU LA SWALI LA MBUNGE VITI MAALUM
na Mwandishi wetu, Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalumu, Thuwayba Idris Muhamed (CUF), ameibana serikali na kuitaka ieleze itawasaidiaje Watanzania ili apate kuelewa fedha iliyokopwa kutoka kwa wahisani imetumika katika mazingira gani.
Mbunge huyo pia alitaka kujua serikali ina uhakika gani kwamba fedha hiyo imefanya kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo.
Akijibu swali la msingi la mbunge huyo, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema fedha zinazokopwa zimekuwa zikitumika kugharamia miradi ya maendeleo hususan miundombinu ya nishati barabara, maji, afya na elimu.
Alisema kuwa fedha zilizokopwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011 na 2011/2012 zilielekezwa katika miradi ya ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa megawati 60 jijini Mwanza na ni euro milioni 61 kutoka HSBC.
Aidha, alisema ujenzi wa kufua umeme wa megawati 100 Ubungo, Dar es Salaam kiasi cha dola za Marekani milioni 103.728 kutoka HSBC zimetumika.
Alisema fedha nyingine zilizokopwa katika kuelekezwa katika miradi mbalimbali ya barabara nchini dola milioni 350 ni kutoka Benki ya Credit Suisse.
Mkuya pia alieleza kuwa serikali ilikopa dola za Marekani milioni 178.125 kutoka Exim Bank ya India kugharamia miradi mbalimbali ya maji, pia zilikopwa dola za Marekani bilioni 1.2 kutoka Exim Benki ya India ya China kugharamia ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na dola za Marekani milioni 230 kutoka Standard Bank kwa lengo la kugharimia miradi mbalimbali ambayo ilikuwa imeainishwa katika bajeti ya maendeleo kwa mwaka husika (Kitabu Vol. 1V), upande wa Tanzania Bara.
Kwa upande wa Zanzibar, Mkuya alisema kuwa Serikali ya Zanzibar ilikopa dola milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kutoka Serikali ya Korea Kusini na dola milioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Zanzibar kutoka Serikali ya Watu wa China.
Pia alisema kuwa dola milioni 42 zilikopwa kwa ajili ya uimarishaji wa sekta ya elimu kutoka Benki ya Dunia, dola milioni 21 zilikopwa kwa ajili ya mradi wa serikali mtandaoni na miradi mingine mingi ambayo ilitekelezwa kwa utaratibu huo.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment