AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 22, 2013

Waziri awakata maini wabunge

NA SHARON SAUWA

22nd April 2013

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka.
Waziri wa  Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, ameungana na wananchi wanaotaka Katiba Mpya iweke kipengele ambacho kitapiga marufuku wabunge kuwa mawaziri.
 
Kabaka aliyasema hayo mjini hapa jana alipokuwa akiwasilisha mada kwenye semina ya wabunge ambao ni wanachama wa Chama cha Wabunge Wanaopambana na Rushwa (APNAC).
 
Semina hiyo ya siku moja, ilikuwa ni ya kuimarisha uwajibikaji na uwazi Tanzania kupitia Katiba mpya na iliandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo Forum Syd.
 
“Mimi naunga mkono hili suala la mawaziri kutokuwa wabunge kwani sababu zinazotolewa ni za msingi, lakini kusema rais asiteue wabunge kwa madai kwamba watashindwa kuwajibika, sikubaliani nalo,” alisema na kuongeza:
 
“Suala la uwajibikaji ni la mtu binafsi kwa sababu hata bungeni unakuta mawaziri hawapo na hali kadhalika, wabunge hawapo wakati wa vikao.”“Pia ieleweke kwamba, mwenye mamlaka ya kumwajibisha yule aliyeteuliwa na rais ni rais mwenyewe, kwa hiyo, nasema tena kwamba, suala la uwajibikaji ni la mtu binafsi,” alisema Waziri Kabaka.
 
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba, alisema wabunge wanapochangia mijadala bungeni, hujali zaidi vyama vyao badala ya wananchi.
 
“Chini ya utaratibu huo, alisema wabunge hao wanaogopa kuporwa kadi za uanachama na makatibu wakuu wa vyama vyao ambao ndiyo wanaowaongoza kila wanapokuwa bungeni,” alisema na kuongeza:
“Waheshimiwa wabunge, mnapokuwa bungeni wakati mwingine mnakuwa na mtazamo fulani fulani kwa sababu mnatetea zaidi vyama vyenu kama ambavyo tumeona hivi karibuni,” alisema.
 
Aliongeza: “Mnapokuwa mle bungeni, kila mmoja anatetea chama chake badala ya kuwatetea wananchi na hili linatokana na ukweli kwamba mnaogopa kunyang’anywa kadi na makatibu wakuu wenu.”
 
Alisema ikitokea mbunge wa CCM anampongeza mbunge mwenzake wa Chadema kwa alichosema bungeni, Katibu Mkuu wa chama atamuita na kumhoji.
 
“Hivyo hivyo kwa wenzetu wa Chadema au NCCR-Mageuzi, ikitokea wakapongeza kauli ya mbunge wa CCM au Serikali, baadaye ataitwa na kuhojiwa, mwenzetu kulikoni?” Alihoji na kuongeza:
“Tunajua Katibu Mkuu anaweza kukupora kadi ya uanachama, lakini mnachotakiwa kufanya ni kuzungumzia masuala ya wananchi wala si vinginevyo.”
 
Pamoja na hayo, aliwataka wabunge watumie muda wao mwingi kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki Katiba mpya.
 
Akifungua semina hiyo,  Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliwataka wananchi wasigawanywe na mchakato wa Katiba mpya kwa kuwa Katiba inaweza kupatikana bila wananchi kugombana.
 
Kwa mujibu wa Spika, wananchi wanatakiwa kuheshimiana wakati wote na kila mmoja anatakiwa kuheshimu mawazo ya mwenzake hata kama yanatofautiana na ya kwake.
 
“Jamani, Katiba mpya ni yetu sote, tusigombane kwa sababu ya Katiba kwa sababu hiyo Katiba inaweza kupatikana hata bila kugombana na kitendo cha kugombana ni dalili ya udhaifu,” alisema Spika.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment