AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 20, 2013

CUF: Hatujihusishi na siasa za vurugu

NA MUHIBU SAID

20th May 2013
Chapa
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakihusiki kuwafundisha wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa na misimamo mikali na kufanya vurugu na kwamba, na kukitupia lawama  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa ndiyo kinahusika na suala hilo.

Kauli hiyo imetolewa na chama hicho kujibu taarifa ya majumuisho ya vikao vya mashauriano vya mikoa (RCC) ya Lindi na Mtwara, vilivyofanyika Desemba, mwaka jana na Mei, mwaka huu.

Vikao hivyo vilihudhuriwa na wakuu wa mikoa na wilaya husika, makamanda wa polisi wa mikoa na wa wilaya na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, wabunge, wenyeviti wa halmashauri na baadhi ya wakurugenzi wa wilaya.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema jana kuwa, taarifa hiyo imeishambulia CUF ikidai kuwa ndiyo chanzo cha misimamo mikali ya wananchi wa mikoa hiyo juu ya masuala ya gesi na mazao ya biashara; kama vile korosho na ardhi. 
Mtatiro alisema wananchi wa mikoa hiyo hawana misimamo mikali, bali ni waadilifu na wanaoipenda nchi yao na kwamba ni watu wazima ambao hawawezi kufundishwa misimamo na chama cha siasa chenye umri wa miaka 20 kama CUF.

“Kama ni misimamo mikali watakuwa wamefundishwa na CCM kwani imeongoza Tanzania kwa nusu karne na hata asilimia 90 ya wabunge na madiwani wa mikoa ya kusini wanatoka CCM, CUF isisukumiwe mzigo usio wake. Manyanyaso, mateso na umaskini wanavyopata wananchi wa kusini vyote vimesababishwa na vinaendelea kusababishwa na CCM, asitafutwe mchawi mwingine,” alisema Mtatiro.

Alisema CUF pia haihusiki na vurugu za wananchi na uvunjifu wa amani uliotokea katika wilaya za Masasi na Tandahimba, mkoani Mtwara na Liwale na Ruangwa mkoani Lindi na kusisitiza kuwa kamwe haitojihusisha na masuala ya siasa za vurugu.

Mtatiro alisema vurugu zilizotokea Masasi zilianza baada ya trafiki kumuomba rushwa dereva wa bodaboda na kwamba, alipokataa na kukimbia, alifukuzwa na polisi na kupata ajali, hali iliyowafanya wenzake kufanya maandamano yaliyosababisha nyumba na mali nyingine kuchomwa moto.

Mtatiro alisema vurugu za Tandahimba zilisababishwa pia na polisi, ambao alidai walichoma moto ofisi ya mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) na kisha kupata ajenda ya kulipiza kisasi kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kuisingizia CUF kwamba, imechoma maduka ya wafanyabiashara.

Alisema vurugu za Liwale zilisababishwa na mfumo mbovu na wa kiuonevu wa stakabadhi ghalani na kwamba, vurugu za Ruangwa zinafanana na za Liwale, ambazo alisema chanzo chake ni wakulima kudhulumiwa fedha zao za korosho.

Hata hivyo, Mtatiro alisema kuhusu msimamo wa wananchi wa mikoa hiyo kutaka gesi ilinufaishe taifa ikiwa palepale Mtwara, hiyo ni sera ya CUF ya muda mrefu.

Alisema CUF haiungi mkono vurugu za wananchi wanapodai haki zao, lakini akaitaka serikali kuwajibika pale wananchi wanapofikia maamuzi hayo, kwani ndiyo inakuwa imezuia haki zao.


CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment