Pemba
Jumla ya miradi tisa yenye thamani ya shilingi 142 milioni imezinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru na kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Juma Ali Simai katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.Akisoma risala kwa kiongozi wa mbio za Mwenge, Ofisa Tawala Wilaya ya Micheweni, Ahmed Khalid Abdalla alisema miradi hiyo ni ile iliyoibuliwa na wananchi na Serikali yenye lengo la kukabiliana na hali ya umaskini na kujiongezea kipato katika familia zao na Taifa kwa ujumla .

Ofisa Tawala huyo alisema kuwa katika kutekeleza shughuli za maendeleo katika Wilaya hiyo , ikiwemo suala la kuhifadhi mazingira kwa kuwashajiisha wananchi kupanda miti kwenye maeneo yao na kusimamia suala la utoaji wa elimu dhidi ya Ukimwi.
Akizindua miradi hiyo , kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Juma Ali Simai aliwataka wananchi kutokubali kugawanywa kwa misingi ya kidini, kisiasa na kikabila bali washirikiane katika shughuli za kujiletea maendeleo .
Alisema kuwa serikali zote mbili ya Muungano na Ile ya Mapinduzi zimekuwa zikichukua hatua za makusudi za kuwaunganisha wananchi kwa kutoa fursa ya kuanzisha vikundi vya ushirika vya ujasiriamali na kuwataka kuitumia fursa hiyo kwa kuanzisha miradi ili waweze kuinufaika na mikopo inayotolewa na serikali zao .
Simai aliwataka vijana kujiepusha na vitendo viovu ambavyo vinaweza kuharibu maisha yao kwa kutojiunga na vigenge vya watumiaji wa dawa za kulevya .
Miongoni mwa shughuli ambazo zimefanywa Wilaya ya Micheweni ni upandaji wa miti , uzinduzi wa kituo cha tiba ya mifugo, uzinduzi wa daraja, ufungaji wa mafunzo ya taaluma ya UKIMWI na dawa za kulevya, kuweka jiwe la msingi kwenye nyumba ya bei nafuu, kuzindua kikundi cha uchomaji wa vyuma, uwekaji wa jiwe la Msingi katika shule ya Mgogoni na kukagua shamba la mkulima Masumbuko.
Chanzo: ZanzibariYetu.
No comments :
Post a Comment