dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 13, 2013

Mauwaji ya Padri Mushi: Mvutano mkali umeibuka Mahakamani

Mtuhumiwa wa mauwaji ya Padri Mushi Bw. Omar Mussa Makame, akiwa mahkamani katika siku ya mwanzo ya usomwaji wa kesi yake.
Mtuhumiwa wa mauwaji ya Padri Mushi Bw. Omar Mussa Makame, akiwa mahkamani katika siku ya mwanzo ya usomwaji wa kesi yake.
Zanzibar,
Mvutano mkali umeibuka Mahakama Kuu ya Zanzibar katika kesi ya mtu anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi Padre Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar.
Upande wa mshitaka na upande wa utetezi katika kesi hiyo inayomkabili Omar Mussa Makame (35) ulivutana kwa hoja mbele ya Jaji Mkusa Sepetu katika Mahakama hiyo iliyopo Vuga mjini hapa.
Upande wa mashitaka ukiongozwa na ofisa kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Abdalla Mgongo ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kwa hiyo kuomba ipangwe siku nyingine.
Lakini, upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Abdalla Juma ulidai kuwa una uhakika kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na hivyo kutaka kesi hiyo isikilizwe au mteja wao aachiwe.
Alidai kwamba hawamuombei dhamana mteja wao kwa vile kesi ya aina hiyo haina dhamana, lakini wanataka aachiwe hadi pale upande wa mashitaka utakapokamilisha upepelezi wake na kufungua kesi mpya.
Alidai kwa mteja wao kuendelea kukaa ndani ni kumnyima haki zake za binadamu na kuiomba Mahakama ioneshe meno kwa kumuachia huru mteja wao.
Jaji Mkusa baada ya kusikiliza pande zote mbili aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 21 mwaka huu atakapotoa maamuzi yake.
Omar aliyegombea ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la  Mlandege katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 alitiwa mbaroni Machi 17 mwaka huu.
Padre Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya mjini hapa.

No comments :

Post a Comment