AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, May 15, 2013

Jumuiya za CCM kuwajengea uwezo Vijana kujinasua na hali ngumu ya kimaisha


Naibu Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania UWT Salma Abuod Talib akifafanua jambo katika Mkutano wa Jumuiya za UVCC, UWT na Wazee na Waandishi wa habari. Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya CCM Zanziba KisiwanduiNaibu Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania UWT Salma Abuod Talib akifafanua jambo katika Mkutano wa Jumuiya za UVCC, UWT na Wazee na Waandishi wa habari. Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya CCM Zanziba Kisiwandui


Jumuiya za Chama cha Mapinduzi UVCCM, UWT na Wazazi zinakusudia kuwajengea uwezo Vijana ili kujinasua na hali ngumu ya kimaisha kwa kuwasomesha kupitia Skuli za Wazazi na Elimu ya Amali ili waweze kujiajiri wenyewe. Zimesema Vijana watakapopata Elimu hiyo itawasaidia kuweza kujiajiri na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira linaloendelea hapa nchini. 
Naibu Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania UWT Salma Abuod Talib ameyasema hayo huko Makao makuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kupongeza mafanikio ya ziara ya kichama iliyofanywa na Dkt. Shein.
Amesema Mafunzo ya Amali yatawasaidia Vijana kuondokana na fikra za kutegemea ajira  Serikalini na kuwawezesha kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea Serikali.

Akizungumzia ziara hiyo Bi Salma amesema ziara ya Dkt. Shein imekuwa na mafanikio makubwa kwani imeweza kuongeza wanachama wapya  jambo ambalo ni ishara ya wazi ya uhai na matumaini ya ushindi wa Chama hicho katika chaguzi za baadae .
Amesema katika hali hiyo kuna haja kubwa kumpongeza kiongozi hiyo kwani ametoa picha ya kufanikiwa kukiimarisha chama na kukiletea maendeleo hapa visiwani na Tanzania kwa ujumla.
“Jumuiya za Chama cha Mapinduzi (UVCCM , UWT na Wazazi) tunampongeza kwa dhati kabisa kuwa mjasiri wa kutembea bila kuchoka na kuwa tayari kutumika kila ambapo alitakiwa ushiriki wake, inaonesha wazi kuwa Makamu Mwenyekiti wetu ni mtu wa watu na anapenda watu pamoja na maendeleo yao” amesema Bi Salma.
Aidha alisema katika ziara hiyo Dkt. Shein alikagua na kutembelea miradi ya CCM ambapo miradi 35 iliwekewa jiwe la msingi na kuziduliwa zikiwemo SACCOS mbali mbali na Vikundi vya Ushirika.
Akizungumzia sintofahamu iliyopo katika baadhi ya Majimbo Bi Salma alisema CCM imepanga kufanya vikao vitakavyojumuisha viongozi wa Majimbo wakiwemo Wabunge na Wawakilishi pamoja na wananchi wao ili kuimarisha utendaji wao.
Amesema vikao hivyo vitatoa mustakabali mzuri kwa viongozi hao na kuweza kuwatumikia wananchi walio wachagua katika hali inayofaa.
Jumla ya Wanachama wapya 5,448 kutoka vyama mbali mbali vya siasa wamejiunga na Chama cha Mapinduzi kufuatia ziara ya Makamo Mwenyekiti wa chama hicho Dkt. Ali Mohammed Shein aliyoifanya hivi karibuni kutembelea mikoa mitano ya Unguja na Pemba kwa lengo la kuangalia na kukipa uhai Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment