dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 13, 2013

Maoni ya Mhariri Annuur: Aliyosema Zitto yazingatiwe

Soma gazeti lako hapa: Annuur Ijumaa

annur** Mtizamo wa akina Anna Abdallah utatuvuruga
AKIFAFANUA Azimio la Bunge juu ya kadhia ya Arusha, Mheshimiwa Anna Abdallah aliitaka Serikali kufuta vikundi vya Kiislamu vyenye dhamira mbaya. Katika kutoa mfano akahoji, inakuwaje Serikali kuandikisha vikundi vya Kiislamu  ambavyo lengo lake ni kupinga Bakwata.
Kwanza, tuseme kuwa hakuna taasisi ya Kiislamu iliyowahi kuanzishwa kwa lengo la kupinga Bakwata. Pili, kama ilivyo kwa taasisi za dini nyingine, ikiwemo Ukristo anaofuata Mheshimiwa Anna, kila taasisi ya Kiislamu inayoanzishwa ni kwa kuzingatia mambo mawili makubwa: Kwanza kutimiza wajibu wa wahusika kwa Mola wao. Kwamba kwa kupitia taasisi hiyo watafanya Da’wah, watahubiri na kuwaletea maendeleo waumini wao na Watanzania kwa ujumla. Pili, wanafanya hivyo kwa kutumia haki yao ya uhuru wa kidini wa kuabudu na kujihusisha na vikundi vya kijamii kama inavyotolewa na Katiba ya Nchi.
Labda swali nije ,kwa nini Anna Abdallah hakuzungumzia utitiri wa taasisi za Kikristo na makanisa yanayochipuka hivi leo ambayo baadhi yao ndiyo yametuletea mgogoro huu wa kuchinja? Kwa nini hakuzungumzia utitiri wa makanisa yanayokera watu mitaani kwa kuimba na kupiga muziki usiku kucha na wananchi wakilalamika ndio kwanza wanaongeza vinanda na magitaa kwa madai kuwa hiyo ni dalili kuwa shetani anakereka kwa hiyo wazidi kumkera?
Anna hakugusa hayo na badala yake ‘kuihami Bakwata’ , si  kuwa anampenda sana Sheikh Al Had Mussa, Mufti Shaaban Simba na Bakwata yao, bali ni kwa sababu fikira inayomwongoza ni ile ile ya Serikali ya kuwabana na kuwadhibiti Waislamu huku Wakristo wao wakitanua watakavyo na taasisi zao. Na haya ndiyo aliyotahadharisha Mheshimiwa Zitto Kabwe bungeni.
Akichangia tarehe 6 Mei katika kikao kinachoendelea Dodoma, Mheshimiwa Zitto Kabwe alitaka Watanzania wasome kutoka yaliyowakuta Ivory Coast na Liberia.
Katika uchambuzi wake akasema kuwa kuna lawama ya muda mrefu sana ya Waislamu kuhusu BAKWATA. Kwamba Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Wanalalamika kuwa wakati Serikali imewapa Wakristo uhuru wa kuwa na taasisi zao huru na haiziingilii, inapokuwa kwa Waislamu, inataka kuwadhibiti Waislamu wote chini ya Bakwata ambayo haina uhalali wowote(Legitimacy) ya kuwasemea Waislamu.
Mtizamo huu, msimamo na mkakati huu wa kuwanyima uhuru Waislamu, ndio uliomfanya Anna Abdallah atoe mfano wa wapinga Bakwata . Anachotaka kuona ni kuwa Waislamu wanarejeshwa katika ile miaka ya Mwalimu Nyerere ambapo Muislamu hakuruhusiwa kufanya jambo lolote la Kiislamu mpaka apate kibali cha Bakwata, na ukienda Bakwata hupati kwa sababu ilishapewa maelekezo.
Hivi tunavyoandika maoni haya kuna Waislamu wanakabiliwa na kesi ya kuchoma makanisa, wengine wapo nje kwa dhamana na wengine kwa zaidi ya miezi sita sasa dhamana zao zimezuiliwa. Makanisa haya ni yale yaliyodaiwa kuchomwa siku ya vurugu za maandamano kupinga hatua ya Polisi kusita kumchukulia hatua kijana aliyekojokolea Qur’an. Mara nyingi panapotokea matukio kama haya, ndipo hupatikana fursa kwa wahalifu nao kufanya yao kama tunavyoona wakivamia na kupora maduka.
Lakini wakati Waislamu wakisubiri hukumu kufuatia kesi hiyo, watu waliochochea waumni wa Kikristo Tunduma wakaandamana na kufanya fujo na kuchoma moto msikiti, taarifa tulizo nazo ni kuwa hakuna mashitaka yoyote waliyokwisha somewa.  Labda swali ni je, ujumbe gani wanapewa Waislamu? Kama mtu anaweza kung’oa dirisha la msikiti na asichukuliwe hatua yoyote na vyombo vya dola, salamu gani anapewa mtu huyu?
Je, kesho na keshokutwa kwa ujumbe huu aliopewa kuwa yeye haguswi, atashindwa kufanya jingine kubwa? Lakini kwa upande, mwingine, katika hali hii, Waislamu waliovunjiwa msikiti wao ambao wanategenea kuwa kuna Serikali yenye kujali usalama wa wnaanchi wote, wanapewa ujumbe gani?
Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Dkt. Emannuel Nchimbi akifunga mkutano wa viongozi wa kidini, jiji ni Dar es Salaam alisisitiza kauli ya serikali ya kukataza mihadhra ya kashfa na kauli za kujenga chuki. Ambalo tungependa lifafanuliwe zaidi, ni hili la mihadhara ya kashfa. Je, kinachokusudiwa nini?
Kumekuwa na mlolongo wa kukamatwa Waislamu wanaokutwa na kanda zenye mawaidha ambapo ndani yake kuna ujumbe wa Qur’an kuwa Yesu si Mungu. Lakini kwa upande mwingine, hatujawahi kuona wauza kanda za kutukuza uungu wa Yesu, wakibughudhiwa. Sasa hapa ni lazima isemwewazi, je kinachokusudiwa hapa ni kupiga marufuku Waislamu kusema kuwa yesu sio Mungu?
Kusema Yesu si Mungu, ni jambo lisilokubalika kwa Mkristo kwa sababu ni sawa na kupinga uungu wa mungu wake Yesu. Lakini pia ni kufru kubwa kwa Muislamu akisikia mtu akisema kuwa Yesu ni mungu. Katika hali hii, ufumbuzi ni nini? Je, ni kuwapiga marufuku Waislamu wasihubiri kuwa Mungu si Yesu ambayo ni sawa na kuwazuiya wasisome baadhi ya aya za Qur’an? Je, wakatazwe wote, Waislamu na Wakristo? Muislamu asiseme kuwa Yesu si Mungu na Mkristo asiseme kuwa Yesu ni Mungu?
Yote haya inapasa yafafanuliwe, vingine itabaki kuwa ni utata mtupu na katika utata huu ndio tunaona Serikali inaungana na Wakristo kuwashambulia Waislamu kuwa ndio wanaotukana na kuwakashifu Wakristo. Wale wanaopiga vijembe vya kuwaombea ‘wenye majini na mapepo’ hawaonekani.
Imekuwa sawa na ile agenda ya ugaidi. Haisemwi kwamba ni kuwapiga vita Waislamu, lakini kila tukio, anayekamatwa ni Muislamu/Muarabu.
Ndio maana hata Arusha tumekimbilia kuwakamata Waarabu wakati Arusha wapo raia wengi wa kigeni. Kwa mtindo huu wasiwasi wetu ni kuwa tutazidi kuivuruga amani ya nchi badala ya kuitengeneza.
Soma gazeti lako hapa: Annuur Ijumaa

No comments :

Post a Comment