NA MWINYI SADALLAH
11th May 2013

Wakati wabunge wakilalamika bungeni kero ya muda mrefu ya wafanyabiashara wanaotoa bidhaa Zanzibar kupeleka Tanzania Bara kutozwa kodi mara mbili, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatetea utaratibu huo.
Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya amewaambia waandishi wa habari mjini Zanzibar katika mahojiano maalum jana kwamba kinachofanywa ni mamlaka kutoza kiasi kilichopungua katika kushusha bidhaa hizo Zanzibar.
Kitilya alisema bidhaa iliyoshushwa Zanzibar hutozwa kiwango cha chini kutokana na utaratibu uliopo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, (SMZ) lakini iwapo bidhaa hiyo itaondoshwa na kupelekwa Tanzania Bara kisheria inapaswa mwenyewe alipe ile tofauti ya kodi.
“Mizigo inayoingia Tanzania Bara kutoka Zanzibar inaangaliwa kodi iliyolipiwa wakati wa kuingia. Iwapo kuna upungufu wa kodi kulinganisha na viwango vinavyotozwa bidhaa hiyo Tanzania Bara, ndipo mfanyabiashara hutakiwa kulipa kodi iliyopungua,” alisema.
Kitilya alisema nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimejiwekea mfumo mmoja wa kodi za bidhaa aina mbalimbali, na huo ndio mfumo unaotumika nchini kote Tanzania.
Alisema bidhaa zote zinazoingizwa nchini huwekwa katika mfumo maalum wa utambuzi ambapo utaratibu huo ndio hubainisha kiasi cha kodi ambacho bidhaa hiyo hupaswa kutozwa.Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya amewaambia waandishi wa habari mjini Zanzibar katika mahojiano maalum jana kwamba kinachofanywa ni mamlaka kutoza kiasi kilichopungua katika kushusha bidhaa hizo Zanzibar.
Kitilya alisema bidhaa iliyoshushwa Zanzibar hutozwa kiwango cha chini kutokana na utaratibu uliopo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, (SMZ) lakini iwapo bidhaa hiyo itaondoshwa na kupelekwa Tanzania Bara kisheria inapaswa mwenyewe alipe ile tofauti ya kodi.
“Mizigo inayoingia Tanzania Bara kutoka Zanzibar inaangaliwa kodi iliyolipiwa wakati wa kuingia. Iwapo kuna upungufu wa kodi kulinganisha na viwango vinavyotozwa bidhaa hiyo Tanzania Bara, ndipo mfanyabiashara hutakiwa kulipa kodi iliyopungua,” alisema.
Kitilya alisema nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimejiwekea mfumo mmoja wa kodi za bidhaa aina mbalimbali, na huo ndio mfumo unaotumika nchini kote Tanzania.
Alipoulizwa kwanini malalamiko ya bidhaa zinazotoka Zanzibar kutozwa kodi mara ya pili zinapoingizwa Tanzania Bara, Kitilya alisema ukweli ni kwamba kinachotozwa kwa bidhaa hizo ni kodi ambayo ilipaswa kulipwa kama bidhaa hiyo ingefika moja kwa moja Tanzania Bara.
“Tunachotoza kwa bidhaa kama hizo ni ile kodi iliyopungua kwa bidhaa hizo kushushwa Zanzibar na siyo kwamba kuna kodi mbili tofauti katika nchi yetu,” alisema Kitilya ambaye anahudhuria mkutano wa makamishna wakuu wa mamlaka za mapato wa Afrika Mashariki unaofanyika Magapwani mjini Zanzibar.
Kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, kulitoka taarifa serikalini kwamba tatizo hilo limekwisha baada ya majadiliano ya ngazi za juu za serikali zote mbili lakini ilielezwa kuwa TRA imeendelea kutoza kodi hiyo licha ya Ofisi ya Makamu wa Rais, kutoa agizo kwa mamlaka hiyo kuacha mtindo huo.
Msimamo huo wa TRA kutoza inachoita “pungufu ya kodi” imesababisha wafanyabiashara wengi wa Zanzibar kuhamisha shughuli zao kwenda Tanzania Bara.
Bidhaa zinazotajwa zaidi kuguswa na utaratibu huo wa TRA, ni magari na vipuri vyake, na vifaa vya matumizi ya umeme majumbani.
Kutokana na Zanzibar kuwa na uchumi mdogo usiolingana na ule wa Tanzania Bara, serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilitoa unafuu wa kodi kwa bidhaa za chakula kama vile mchele, unga wa ngano na sukari ambazo hutozwa kodi ya asilimia 12.5 badala ya asilimia 25 (kwa sukari na ngano) na asilimia 75 kwa mchele kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kuhusu mkutano huo, Kitilya alisema lengo lake kubwa ni kujitathmini kiutendaji na kuangalia nchi wanachama zimefikia kiasi gani katika malengo yao ya ukusanyaji wa mapato.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment