NA MWANDISHI WETU
10th May 2013
(1)(3).jpg)
Wanafunzi wa ngazi mbalimbali ikiwemo vyuo vya walimu nchini, watanufaika na ujio wa wataalamu wa elimu kutoka nje kufundisha lugha ya Kiingereza.
Wataamu hao kutoka Uingereza watakuja nchini kufutia mradi wa mafunzo ya lugha ya Kingereza unaofadhiliwa na Taasisi ya elimu ya kingereza (British Council), VSO kwa kushirikiana na serikali za uingereza na Tanzania.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, wakati wa uzindizi wa mradi huo unaojulikana kama Mradi wa Uboreshaji wa Elimu (EUIP-T ELT) unaolenga pamoja na mambo mengine, nyanja ya mafunzo ya lugha ya Kingereza.
“Hii ni moja kati ya hatua ambazo wizara imelenga kuzitekeleza ili kuboresha suala la elimu nchini, hivi sasa tunazo shule nyingi, lakini bado tumekuwa na changamoto katika suala zima la kuiboresha elimu yetu ili kukidhi viwango,” alisema.
Waziri Kawambwa alieleza kuwa mradi huo utatekelezwa kwa miaka minne na utagharimu fedha za Paundi milioni 60 (Sh. bilioni 149).Wataamu hao kutoka Uingereza watakuja nchini kufutia mradi wa mafunzo ya lugha ya Kingereza unaofadhiliwa na Taasisi ya elimu ya kingereza (British Council), VSO kwa kushirikiana na serikali za uingereza na Tanzania.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, wakati wa uzindizi wa mradi huo unaojulikana kama Mradi wa Uboreshaji wa Elimu (EUIP-T ELT) unaolenga pamoja na mambo mengine, nyanja ya mafunzo ya lugha ya Kingereza.
“Hii ni moja kati ya hatua ambazo wizara imelenga kuzitekeleza ili kuboresha suala la elimu nchini, hivi sasa tunazo shule nyingi, lakini bado tumekuwa na changamoto katika suala zima la kuiboresha elimu yetu ili kukidhi viwango,” alisema.
Alifafanua kuwa mradi huo unalenga kuwanufaisha wanafunzi wa sekondari 700,000, wa shule za msingi 35,000, walimu wanafunzi 70,000; wakufunzi 1,650, wakuu wa taaluma 510, vyuo vya serikali 34 na wakaguzi 54.
Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Kingereza (British Council), Sally Robinson, alieleza kuwa mradi huo unalenga kuwaandaa walimu pamoja na wanafunzi, ili wajue vyema lungha ya Kingereza katika kujifunza na vilevile kuwafundisha wengine.
“Kutokana na ushindani wa soko huria na mwingiliano wa kimawasiliano, sisi tumedhamiria kwa dhati kuboresha elimu ya Tanzania hususani katika kutoa mafunzo ya lugha ya Kingereza yenye kuzingatia viwango na ubora,” alisema.
Mwakilishi wa serikali ya Uingereza, Liz Tayler, alisema Uingereza itahakikisha inashirikiana kikamilifu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kuwaleta wataalamu wa lugha hiyo, msaada wa kifedha pamoja na zana za kazi.
“Sisi tunatoa walimu wenye sifa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vya ualimu wenye sifa,” alisema.
Waziri Kawambwa alisisitiza kwamba jamii itambue kuwa wahitimu wa kidato cha nne wa mwaka jana ambao matokeo yao yamefutwa, hawatarudia mtihani wala mtihani kusahihishwa upya kama inavyodhaniwa na wengi, isipokuwa kinachofanyiaka ni kubadilisha utaratibu wa madaraja uliotumika katika kupanga matokeo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment