AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 29, 2013

Uvccm Zanzibar wamfananisha Wakili na Mandela

NA MWANDISHI WETU

29th June 2013


Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela.
Jumuiya ya UVCCM imemfananisha Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Zanzibar hayati Idris Abdul Wakili  na Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa  UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja, Salha Mohamed Mwinjuma, mara baada ya  ujumbe wa UVCCM kumaliza kuzuru kaburi lake Makunduchi Kisiwani Unguja jana.

Salha alisema hayati Wakil aliingia madarakani mwaka 1985 mara baada ya Rais Ali Hassan Mwinyi kuondoka na kukaa katika uongozi kwa kipindi kimoja,  baadae akamwachia Dk Salmin Amour.

"Huyo ni Mandela wa Afrika Mashariki na Kati, hakutaka kung'ang'ani madaraka, aliheshimu umri wake na kuamua kumpisha mgombea kijana, ni kama Mandela aliyekaa gerezani kwa miaka 27 na madarakani kwa kipindi kifupi akijiondoa," alisema Mwenyekiti huyo wa UVCCM.

Aliwataka viongozi wengine Afrika kuiga mfano wa hayati Mzee Wakil ambaye hakuweka mbele madaraka na kwamba amekufa na kuiachia heshima ya aina yake Zanzibar.

Aidha alisema itakuwa ni busara kwa Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad naye akaiga mfano huo wa kustaafu siasa ili kuwapisha vijana wanaochipukia kuongoza CUF na kugombea urais.

Akizungumzia mfumo wa Muungano , Salha alisema ni hatari kufanya majaribio au kutaka kuyaweka rehani maisha ya watu na maendeleo yao kwa kutoa madai magumu  au kuwaghilibu wananchi kutaka Muungano wa mkataba.

Alisema msingi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kuwepo kwa umoja, utulivu na kuimarika kwa mahusiano watu wa pande mbili hivyo ni vyema kero na malalamiko kushghulikiwa na kutatuliwa kuliko kuvunja Muungano.
 
CHANZO: NIPASHE

2 comments :

  1. HUYU MWANADADA ANAMJUA MANDELA AU ANAMSIKIA KWENYE VYOMBO VYA HABARI MANDELA NI SHUJAA WA WATU NA MFANO ULIMWENGU MZIMA MPATANISHI HANA CHUKI WALA HAPOKEI FITNA MSTAHAMILIVU NA MSAMEHEVU.SINA NIA YA KUMPONDA AU KUMKASHIFU MZEE IDIRISA LA HAPANA HAKUWA MTU MUOVU SOTE TUNA MJUA NI MCHA MUNGU.ALIKUWA ANAKUJA KUSWALI SANA TU HAPA MSIKITI WA KWA BOKO SALA ZA LAASIRI NA TARAWEIH KWA IMAMU WETU SHEIKH YUSSUF MOHAMMED KHAMIS.TUKIZUNGUMZIA UWANJA WA SIASA HUWEZI KABISA KUMFANANISHA NA MANDELA NA WALA HATATOKEA KIONGOZI BORA AFRIKA KAMA MANDELA.
    BAADA YA YA JUMBE KUONDOLEWA KWENYE UONGOZI AKAJA ALI H. MWINYI KWA MUDA MCHACHE TU KAMA MWAKA MMJA NA USHEI HIVI HALI IKABADILIKA SANA NEEMA IKAONEKANA MVUA MAZAO NJAA IKAPUNGUA BIASHARA IKANOGA HALI IKAWA SHWARI WATU WAKIPENDANA ,WAKISHIRIKIANA WAKISAIDIANA YAANI RAHA MUSTAREHE.NYERERE AKANG"ATUKA MWINYI AKAWA RAISI WA TANZANIA NA MZEE IDIRISA AKAWA RAISI WAZNZ ,KUMBUKA KABLA YA URAISI ALIKUWA SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA BENZI YAKE NYEUSI.WAKATI HUO HUO SEIFU SHARIFU AKIWA WAZIRI KIONGOZI KAMA SIKOSEI,HAPO SASA FITNA IKARUDI UPYA .AKAFITINISHWA SHEIKH IDIRISA NA WAZIRI KIONGOZI WAKE FITNA ZILITOKA DODOMA NA SEIF AKAFUKUZWA CHAMANI NA SERIKALINI NA AKAWEKWA JELA.NA HAPO HAPO UHUSIANO MZURI BAINA YA WAPEMBA NA WAMAKUNDUCHI UKAFIKA KIKOMO NA BAADAE IKAWA UHASAMA PEMBA NA UNGUJA NDIO HII FITNA INAYOTUSUMBUA MPAKA LEO IMEANZIA DODOMA IKAJA PEMBA NA MAKUNDUCHI IKAZAA UUNGUJA NA UPEMBA HUO NDIO UKWELI NIMEYAONA KWA MACHO YANGU SIMLAUMU MTU KWA SABABU SOTE TUMESHIRIKI MAMBO HAYA KWA NJIA MOJA AU NYENGINE KWA KUJUA AU KUTOKUJUA.KAMA MNA KUMBUKUMBU WAPEMBA NA WAMAKUNDUCHI WALIKUWA MASWAHIBA WAKUBWA SANA WALIOZESHANA NA KUPEANA WATOTO KULEA HALIKADHALIKA WAUNGUJA NA WAPEMBA KIUJUMLA LAKINI HUU UHUSIANO WA WAPEMBA NA WAMAKUNDUCHI ULIKUWA SPESHELI TOKEA ENZI NA ENZI KWA BAHATI MBAYA UKAFA KIPINDI HICHO CHA SHEIKH IDRIS NA MAALIM SEIF MIMI SI MPEMBA WALA SI MMAKUNDUCHI NI MUUNGUJA TU WA FUONI NA UZINI ILICHOBAKI NI KUSAMEHEANA WAUNGUJA NA WAPEMBA SOTE NI WAZANZIBARI TURUDISHE MAHUSIANO YETU TUJENGE NCHI YETU.HUO NDIO MTIHANI ULOMKUTA SHEIKH IDRISA NA MAALIMU ATHARI ZAKE ZINATUTAFUNA MPAKA LEO.VIPI UTAMFANANISHA NA MANDELA KISIASA?
    HUYU ANAEMFANANISHA SHEIKH IDRIS NA MANDELA NDIO HAWA WANASIASA UCHWARA HAWAJUI HATA MATATIZO YANAYOIKABILI JAMII WAO WANAROPOKWA TU KWA KULINDA MASLAHI YAO NA WAPO WENGI SANA HAWA NDIO MAANA HATUENDELEI ,HUEZI KUTATUA TATIZO BILA YA KULIJUA TATIZO LENYEWE


    ReplyDelete
  2. Assalaam alaykum
    Maalim wangu uliyetoa maoni hapo juu, ahsante sana kwa maoni yako, kwa kweli umenifanya nitokwe na machozi, mimi ni kijana mdogo kiasi , ila nakumbuka hayo uliyoyasema ya udugu baina ya watu wa visiwa hivi, hakukuwa na taabu yoyote baina ya muunguja na mpemba kiasi hicho, hizi fitna zimepandikizwa na hao wanasiasa uchwara wanaopnda maslahi yao binafsi.
    Mola atulinde na kila baya, aturudishie umoja ,upendo ,ushirikiano wetu kama zamani amiin.

    ReplyDelete