NA MWANDISHI WETU
1st August 2013
Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Benki ya Azania, Bernard Haule, wakati akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles Singili, wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo maalum kwa wateja wake Waislamu jijini Dar es Salaam juzi.
“Tupo katika maandalizi ya kuanzisha huduma za kibenki kwa niaba ya wateja wetu ambao ni waumini wa dini ya Kiislaamu baada ya kuanza kutoa huduma kupitia mawakala miezi michache iliyopita," alisema.
Aliongeza: “Tunaamini huduma hii itasaidia kuleta ahueni kwa wateja wetu Waislamu. Dhamira yetu ni kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma za kipekee zitakazokidhi matakwa yao kikamilifu.”
Haule alisema kuwa benki yake imekuwa ikiandaa hafla za kufuturisha kwa wateja wake jijini Dar es Salaam na mikoa mingine ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kujumuika pamoja na wateja wake hususani wakati huu wa Ramadhan.
Alisema kuwa benki yake imekuwa katika mstari wa mbele wa kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii kupitia mpango wake wa kuisaidia jamii hususani katika masuala ya afya na elimu.
Aidha, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, wakati wa hafla hiyo aliwaasa Waislamu wote nchini kuungana pamoja na kufuata misingi ya dini ya Kiislamu.
“Waislamu inatakiwa watumie mwezi huu wa Ramadhan kwa kuzidisha upendo miongoni mwao. Na upendo huu usijengeke kwa Waislamu pekee bali hata kwa wasio Waislamu," alisema.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment