Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 4, 2013

RASIMU YA KATIBA!

Rasimu ya Katiba: Wapendekeza Rais wa Zanzibar awe Makamo wa Rais

4th August 2013


Tume yamabadiliko ya Katiba imetakiwa kufutamapendekezo yanayoruhusu mgombea binafsi na kurudisha utaratibu wa zamani Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mapendekezo hayo yametolewa na kundi namba moja la Baraza la Katiba kutoka Wilaya ya Magharibi wakati wa kiwasilisha kazi ya makundi ambapo kundi hilo lilipewa kazi ya kujadili mihimili ya dola katika baraza hilo linalofanyika mjini hapa.
Akiwasilisha ripoti, Katibu wa kundi hilo Khairallah Tawaqal (Bububu), alisema kwamba ibara ya 77 ambayo inaruhusu kuwapo kwa mgombea huru iondolewe kwa vile kitendo cha kuruhusu wagombea binafsi kunaweza kuibua mgogoro hasa wanaposhindwa kutimiza majukumu yao.
Khairallah alisema mgombea huru anaweza kuleta migongano ya kiutendaji na kutosimamiwa kinidhamu katika uwajibikaji wake tofauti na mgombea anayepitia vyama vya siasa.
Alisema masharti ya mgombea urais yabakie kama ya livyo isipokuwa kifungu kinachozungumzia lazima awe na akili timamu kiongezwe na kusomeka awe mwenye afya njema kabla ya kusimamishwa kuwa mgombea wanafasi ya urais.
Akisoma mapendekezo ya kundi hilo alisema ibara ya 89 iangaliwekwa umakini na kurejesha utaratibu wa zamani wa kikatiba ili Rais akitokea upande mmoja wa Muungano na makamo wake atoke upande wapili pia majimbo ya uchaguzi ya bakie kama yalivyo chini ya serikali mbili.
Alisema mfumo huo utapunguza idadi kubwa ya viongozi wakitaifa na gharama za uendeshajinakubakisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamo wa Rais toka upande mmoja wa Muungano na Waziri Mkuu.
Hata hivyo mjumbe kutoka Chukwani Hassan Mussa Mohamed alitofautiana na wenza na kusisitiza msimamo wake wakutaka masuala hayo yaondolewe katika orodha ya muungano.
Awali mjumbe Mwanaisha Khamis (Kiembesamaki) alitaka viti maalum vya ubunge viendelee kubaki kama vilivyo badala ya kufutwa kwa vile vitaongeza shime ya uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi.
Tume ya mabadiliko ya katiba inatarajia kuendelea na kazi zake za kukutana na mabaraza ya katiba kwa kukutana na kundi la walemavu baada ya jana kukamilisha kukutana na wajumbe wawilaya tano kati ya sita za kisiwani Unguja.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment