4th August 2013
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Uenezi wa Habari wa chama hicho, Abdul Kambaga, akiongea na NIPASHE jijini Dar es Salaam.
Alisema chama chake kimeaandaa vijana watakaolinda amani kwa viongozi wao ili kuwaepusha na mabomu, wakati wa mikutano na maandamano hayo.
“Serikali kwa kutumia polisi inawapiga wapinzani, CUF hawatuwezi, tutaandamana, tutafanya mikutano nchi nzima, alisema Kambaya.”
Katibu huyo wa Uenezi wa Habari, alifafanua kuwa chama chao kimesajiliwa kisheria na kipo kwa mujibu wa katiba ya nchi, hakioni sababu yakuzuiwa na polisi kila wanapotaka kufanya mikutano yao kwa kisingizio kuwa Mtwara hakuna amani hata baada ya tatizo la gesi kuisha.
Alisema kuwa chama chake kina vijana waliosajiliwa kisheria kwa shughuli za chama kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa nchini, akadai kuwa CUF haioni sababu yakutofanya maandamano na mikutano kwani bado viongozi wa chama hicho wanakamatwa, wanapekuliwa na polisi bila sababu.
Hivi karibuni CUF kilizuiwa kufanya mikutano ikiwa ni pamoja na maandamano hasa mkoa wa Mtwara kutokana na tatizo la gesi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment